Waraghbishi
toka vijiji vya Iponya, Nyakasumula, Bukandwe na Shenda wakiwa katika picha ya pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Shenda.
Ni miaka mitatu na miezi nane
toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na
Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu
ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya,
Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita. Ni katika mazungumzo hayo ya siku tatu,
ambayo Fedson toka kijiji cha Shenda alibadilishwa na kuwa mraghbishi wa
aling’amua uwezo alio nao katika kusimamia rasilimali za kijiji chao, suala ni angezisimamiaje
wakati yeye si kiongozi na ni jukumu la wanakijiji
wote. Katika mazungumzo hayo rafiki yao, Chukua Hatua aliwaambia, “Ni jukumu lako
Fedson na waraghbishi wengine mliopo hapa, ni jukumu lenu la msingi kuj i t aj
i r i sha kwa taarifa na maarifa. Kwa kufanya hivyo mtakuwa na uwezo wa kujenga
hoja mkizithibithisha na vielelezo.
Hivyo ni jukumu lenu kujua ni wapi na toka
kwa nani mtapata taarifa na vielelezo vya hoja yenu. Uzito wa hoja na maelezo
kwa uthibitisho ni silaha muhimu kama mnataka kushawishi wenz e n u k u c h u k u a hatua.” Baada ya maelezo hayo walitakiwa kwenda
kutembelea halmashauri ya wilaya yao, wakati huo ikiitwa Bukombe. Na baadhi ya maeneo
hayo ni ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri. Maelezo haya yalilenga
katika haki ya kupata taarifa, kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba.
“Kweli mazungumzo hayo
yalinijengea uwezo mkubwa sana, Chukua Hatua alinipatia muongozo na akanipangia
kwenda kwa mkuu wa wilaya. Moja kwa moja nikaonana na DC nikaanza kumuhoji
mambo mbalimbali kuhusu pembejeo. Ingawa majibu aliyonipa sikuridhika nayo, lakini
nilishukuru kupata nafasi ya kuongea naye. Na kwa kweli tokea siku hiyo nikawa
na ujasiri mkubwa sana,” Fedson Yaida akitoa ushuhuda wa siku ambayo uoga ulimtoka.
Ujasiri huo wenye msukumo wa ndani
toka kwa mraghbishi mmoja kwenda kwa wenzake kwa njia ya kuwashirikisha aliyopatiwa
na Chukua Hatua, ndio umekuwa chanzo kikubwa cha mafanikio ya pamoja ya wana
Shenda katika kusimamia rasilimali zao. Safari ya mwandishi katika kijiji cha Shenda
ilimtia moyo sana. Alikutana na waraghbishi toka vijiji vya Shenda, Ipoja, na Buluhe.
Mkusanyiko huu ulikuwa na watu wa kada mbalimbali; walimu, wajumbe wa serikali ya
kijiji, wazee, na wakulima. Aliwakuta wakiwa pamoja na Mwenyekiti na Mtendaji
wa kijiji chao. Na wote kwa pamoja walikuwa wanazungumzia mustakabali wa
maendeleo ya kijiji chao. Na kwa haraka aligundua wote wamekuwa waraghabishi,
akajiuliza aliyekutana na Chukua Hatua alikuwa mmoja, lakini sasa wapo kwa
makundi na wote wanajitambulisha kama waraghbishi. Hamu na shauku yao ya kutaka kusimamia rasilimali
zao ndio imekuwa nguzo kubwa ya wao kuweza kufuatilia matumizi ya vyanzo vya
mapato ya kijiji chao. Ni miaka miwili imepita toka wananchi hao wautoe uongozi
wa kijiji madarakani kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha. Kwa pamoja waliongozana
na mwenyekiti wao pamoja na mtendaji wa kijiji na mpaka ofisi ya kata na
kuwakabidhi kwa polisi. Ubadhirifu huo ulithibitishwa na taarifa ya ukaguzi,
iliyoonyesha upotevu wa kiasi cha shilingi milioni mbili laki tisa na elfu hamsini
(2,950,000/-). Taarifa hiyo ilisomwa katika mkutano wa hadhara na viongozi
kutakiwa kulipa pesa hizo ambazo walizirudisha.
Baada ya hapo walichagua uongozi mpya;
mwenyekiti na halmashauri ya serikali ya kijiji na Mkurugenzi wa wilaya
akawaletea mtendaji mpya wa kijiji. Na huo ndio ukawa mwanzo mpya wa safari ya
uraghbishi katika kijiji hicho. Vuguvugu hilo la mapinduzi liliongozwa na waraghbishi
wapya waliowezeshwa na Fedson wakisaidiana na rafiki yake wa karibu Abdu Haridi
ambaye pia ni mraghbishi. Habari ya
kutolewa madarakani kwa uongozi wa kijiji hicho ilirushwa pia na redio ya
Kahama FM na kupelekea mkuu wa wilaya kumtuma mwakilishi wake akaongee na wananchi
wa kijiji cha Shenda. Uungwaji
mkono huu na Mkuu wa Wilaya ni
dalili kwamba yupo tayari kufanya
kazi na wananchi wa kijiji cha
Shenda. Yeye ni kiongozi wao na dhahiri anawajibika kwao kama ambavyo kiongozi
yeyote anayejali watu wake angefanya. Kwa sasa wanashirikiana kwa pamoja na uongozi
mpya na mwandishi alithibitisha hivyo kwa kuwa alipata fursa ya K a m a
mwanzo mpya, wamekubal i ana kufanya ujenzi wa ofisi mpya ya kijiji.
K wa n z
a wa meanza na ujenzi wa zahanati kwa k
u k a m i l i s h a msingi wake. Na wananchi wamekubali kuchangia, kila kaya
matofali 50 na wengine w a m e c h a n g i a mawe. Uhai umerudi tena na kila mtu
ana shauku ya kufanikisha ujenzi huo. Lakinisi hivyo tu wanataka kukamilisha pia
na ujenzi wa zahanati ya kijiji. Haya yote yakiwa ni matunda ya ushirikiano
kati ya uongozi wa kijiji na waraghbishi na wanakijiji wote kwa ujumla. “Tumekaa muda mrefu sana bila zahanati hasa
kwa ajili ya kina mama. Ni kilometa tano kutoka hapa mpaka zahanati ya jirani.
Na kijiji chetu kama unavyokijua, hakina teksi, labda tumbebe kwa tela la ng’ombe
au punda kama huna baiskeli. Tukajiuliza kwanini tusiiambie serikali yetu
tujenge zahanati hapa karibu,”anafafanua Abdi Haridi. Lakini si hivyo tu Mwenyekiti ameshahamasisha kila
mwananchi achangie mawe, achangie matofali. Kwa sasa wameonela kumalizia kabisa
ofisi yao ya kijiji. Ya sasa ipo katika hali mbaya harufu ya kinyesi cha popo
na jengo lenyewe lina nyufa ikinyesha mvua kubwa itakuwa ni shida inaweza hata
kuanguka na hapa ndio makao makuu ya kijiji.
Kwa hiyo nguvu zao sasa ni kukamilisha
hii ofisi afu ndio waendelee na zahanati ya kina mama. Mazungumzo hayo na Chukua Hatua yalifanyika
katika mfumo wa mafunzo yaliwawezesha
waraghbishi toka vijiji vya Ipoja, Shenda, Buluha na Nyakasaluma kuanza
kufuatilia na kuhamasisha wengine kufanya hivyo pia. Si kitu
kirahisi sana kuwa mraghbishi, kunahitaji kujiamini, kujitambua na moyo wa
kujitolea pia.. Katika kijiji cha
Nyakasaluma wananchi walihamasishwa na uongozi wao kuchangia pesa kwa ajili ya
ujenzi wa Zahanati na kwa kweli walichangia kila
kaya ilitoa kiasi cha shilingi za kitanzania elfu saba mia tano. Swali la
kujiuliza michango ya maendeleo ya namna hii, inaamuliwaje? Wananchi
wanahusishwaje? Je, wamefanya utambuzi wa watu/kaya/familia uwezo walio nao?
Kwa mujibu wa mraghabishi Patrick Matagale ujenzi ulianza lakini ghafla
ukasimama na walipofuatilia ikaonekana kwamba ujenzi hautaendelea kwa madai
kwamba mwekezaji wa kijiji atamalizia na wananchi pesa wameshachangia. “Sasa
ilikuwa ni kuhoji tu kuhusu ile pesa iliyochangwa na wananchi”, anasimulia mraghbishi
Patrick. Uaminifu ni silaha kubwa ya
uongozi imara, na mara watu wanaposhindwa kukuamini kama kiongozi, huamua
kuchukua njia yao ya kutokukupa dhamana ya kuwaongoza, “Hivyo
tulichoamua kufanya kwa sasa ni kwamba hatutachangia tena pesa na badala yake
tunahamasisha watu kuchangia vitu badala ya pesa, kama walivyofanya wenzetu wa
Shenda. Mwenye mawe, matofali, mbao na chochote kile alete,” anafafanua
mraghbishi Patrick Matagale toka kijiji cha Nyakasaluma. Katika
kijiji cha Iponya, suala
lililoibuka ni michango
wanayochangishwa wananchi. Ambapo kila kaya imetakiwa kuchangia kiasi cha
shilingi za kitazania elfu sita (6,000/) kwa ajili ya mradi wa maji wa visima
virefu. Mradi huu unafadhiliwa na benki ya dunia na una thamani ya shilingi za kitanzania
milioni 221/-
Hivyo wananchi nao wametakiwa kuunga mkono juhudi hizo kwa kuchangia
pia gharama za ujenzi huo na wananchi walikubali bila kusita na kwa ujumla wao
walichangia kiasi cha shilingi za kitanzania milioni tatu (3,000,000/-). “Cha kushangaza wananchi wameshachanga hela
zao, ila mpaka muda huu naongea hakuna ambacho kimeshafanyika. Lakini kwenye
muhadhara tulidanganywa kwamba mradi ukishaanza Shenda na sisi pia tutaanza
kufaidika, mpaka dakika hii hakuna maji,” anafafanua Thomas Mlekwa toka katika kijiji cha Iponya. Wananchi wakawa wanataka kujua nini kimetokea
baada ya wao kuchanga, kama anavyosimulia mwana mama Leornada Mathias toka kijiji
cha Ipoja, “Ilikuwa mishe mishe kweli, kila siku mwenyekiti anapita katika kaya
anahamasisha watu wachangie ili tuondokane na tatizo la maji. Ni kweli
tuliitikia tukatoa michango na tuliambiwa tukichelewa tu huu mradi unatupita.
Tukafungua akaunti na fedha zikawekwa. Baada ya hapo tukaona kimya kabisa.” Katika mikutano ya hadhara ya kijiji iliyofanyika
hapo wananchi walitaka kujua nini kimetokea kwani fedha tayari kiasi cha
shilingi za kitanzania milioni tatu zimeshawekwa benki.
“Kwenye mkutano watu wakataka kujua meza
imekuwaje tuliambiwa Shenda wakipata maji
na sisi pia, mbona tayari kwa wenzetu yapo.
Ndio tukaja kujua kwamba hakuna mradi wa maji. Na badala yake viongozi
wanatuambia kwamba ile fedha wanaanza kuisoma kwenye mapato na matumizi,”
anaendelea kufafanua Leornada. Na katika
muda huo wakaambiwa kwamba tayari laki nne zimeshatumika kutokana na makato ya
gharama za kuendesha akaunti. Kwa hiyo uendeshaji wa akaunti umekula mpaka sasa
kiasi cha milioni mbili na laki tatu zimebaki laki saba tu. Hapa pana kazi kubwa
ya kufanya.
Pamoja na Shenda kuonekana kwamba
kwao maji yameshaanza kutoka katika mabomba, bado kuna changamoto nyingi za kuwezesha
kukamilika kwa mradi huo wa maji. Na waraghbishi wapo mstari wa mbele
kufuatilia nini kinachoendelea kwenye mradi huo. Ni mradi ambao waliomba
wapatiwe na utekelezaji wake umeshaanza ingawa baadhi ya maeneo bado hawapati
maji. “Mradi huu wa maji ni sawa na hakuna. Sisi
wananchi wa Shenda tumechangia nguvu zetu. Tumechangia asilimia yetu
tuliyoambiwa na serikali. Serikali ikachangia asilimia yake, ina maana kilikuwa
ni kisima tu cha vitongoji vine vya kijiji chetu. Tuna tenki lile pale
limeshakamilishwa. Mashine ipo kule
kwenye chanzo cha maji. Italike kule, lakini kijiji kizima kuna gati nane tu.
Kuna vitongoji vingine havina gati. Kitongoji kizima kinapewa gati moja ebu niambie
kitakidhi wangapi?” anauliza Abdi Haridi mraghbishi wa Shenda.
Gati zilizopo Shenda zinatokana
na waraghbishi na wananchi kufuatilia suala hilo kwa karibu. Kwa sababu ni kitu
walichokiomba wapatiwe na serikali. Baadhi ya vitongoji vya kijiji hicho
vimetenganishwa na barabara. Hivyo wametaarifiwa kwamba gati haiwezi kuvuka barabara.
Ili hali kwa baadhi ya viongozi wao gati imevuka barabara,” mraghbishi Abdi anauliza,
“Lakini ukienda pale makao makuu ya kata
pale unakuta gati imewekwa kwa kiongozi. Nikauliza swali pale mbona kule Shenda
tumeambiwa gati haiwezi kukata barabara ndio maana wananchi wa upande wa pili
wa kijiji hawapati maji. Imekuwaje kwa kiongozi imekata barabara na kuingia
mpaka mgongoni mwa nyumba yake? Barabara ile ile niliyoambiwa gati haiwezi
kukatiza ndio hiyo hiyo imetumiwa kukatiza gati.” Kaloras Majura, mraghbishi
kutoka kijiji cha Bukandwe kutoka kata yenye jina hilo hilo la Bukandwe, pamoja
na kwamba yeye ni mraghbishi lakini pia alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya
shule ya msingi ya kijiji chao.
“Changamoto niliyoanza nayo ilikuwa ni pale
shule, nilipogundua kwamba mwalimu mkuu anaitisha michango, bila kuwashirikisha
wazazi. Pamoja na nafasi niliyokuwa nayo lakini pia nilikuwa natoa elimu kwa
wananchi. Nikajengewa kampeni na kufanyiwa uhasama na mwisho wa siku nikaambiwa nafasi ya uenyekiti hainifai,
kwa sababu natoa siri. Hivyo nimebaki mjumbe tu,” katika hali ya upole anaelezea
mraghbishi Majura.
Suala lingine ambalo
limejitokeza ni kuhusu mganga wa zahanati ya kijiji cha Bukandwe, ambaye
alikuwa akiwachangisha wananchi kiasi cha shilingi za kitanzania elfu kumi
(10,000/-) za mfuko wa afya. Alichokuwa akifanya wakati anawaandikia alikuwa
akiweka kumbukumbu tofauti za mwaka. “Kama mtu katoa hela mwaka huu yeye
anamuandikia katoa mwaka 2012 na wengine mwaka 2013. Baada ya muda
akawa amehamishwa sasa watu wanapokwenda pale zahanati wanaambiwa kwamba wewe muda
umeshakwisha ulitoa mwaka juzi hivyo uanze upya,” anasimulia Majura Kutokana na nafasi yake ya uraghbishi Majura ameweza
kukaa na kamati ya kijiji ya afya. Na ameishawishi kamati kuwasiliana na watu
waliolipa kuandaa vielelezo vyao na kufanya mawasiliano na mganga mkuu wa
wilaya, ili waweze kujua wanachukua hatua gani kuhusu huyo mganga. Lengo la
kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba wananchi wanarudishiwa fedha zao walizochanga.
Si kitu kirahisi sana pia kufanya
uraghbishi kwa sababu mara kadhaa waraghbishi wamekuwa wakitishiwa tishiwa ili
wasiulize ulize maswali na kuhamasisha wananchi , lakini bado mambo yameendelea. “Sisi waraghbishi tunapata muda mgumu sana
tunakutana na watu tofauti na viongozi tofauti. Tunatishiwa amani, ila na sisi
tutapambana kama tulivyokwisha kupambana mpaka dakika ya mwisho ili haki yetu
ipatikane. Tukianza kuyatafuta mashirika ili tushirikiane nayo katika kuweka mambo
sawa, kama hivi. Tayari tunaonekana siye wabaya kwa wale viongozi wa juu.
Kwamba sisi tunawapondea wale. Basi sisi tunaomba waje wale wakubwa zaidi, waje
watuulizie nini kinaendelea ili tuwaambie ukweli,” anaeleza kwa kujiamini mraghbishi
Abdi Haridi wa Shenda. Harakati hizi zinaungwa mkono na mwenyekiti wa
kijiji cha Shenda, Masumbuko Kwileka, kama anavyosema kuhusu warghabishi, “Kila siku waraghbishi tunao hapa. Fedson huwa
anakujaga hapa wanazunguka huko na kijana wake huyu hapa Haridi. Wanapita
vijiji hadi vijiji wanahamasisha.Hivyo waraghbishi wana hamasa hata mwenyekiti
ajaye atakayekuja watakuwa msaada kwake. Manake watamuuliza tu sasa mkuu unakwendaje
hapa na itabidi uwaeleze mambo yanakwendaje. Hivyo mnapopata pesa ni lazima
umuelezee mraghbishi zinavyokwenda.” Ni
mwaka sasa umepita toka shuguli za Chukua Hatua zisimame kwa muda, ila cha
kufurahisha ni waraghbishi wameendelea na harakati za kujiletea maendeleo kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali hasa wananchi wenzao. Na si hivyo tu wameendelea
kuwatengeneza waraghbishi wengine ambao na wanaendeleza harakati za kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment