Monday, December 7, 2015

Onesho la Pop Up Bongo kufanyika hivi karibuni

Mmoja kati ya wanawake wajasiriamali jijini Dar, Aika Lawere ambaye pia ni mmiliki wa Mbezi Garden alikuwepo pia.
Mwanzilishi mwenza wa Pop Up Bongo, Natasha Stambuli akionesha bidhaa za duka lake la Secret Habit ambalo nalo lilionesha bidhaa zake siku hiyo.
Mbunifu wa mavazi nchini wa lebo ya Branoz Collection, Bahati Kombe (katikati) akipanga bidhaa zake wakati wa Tamasha la Pop Up Bongo lililofanyika juzi Trinity Oysterbay chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff.
Meneja chapa (pombe kali) wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Wauzaji wa bidhaa mbalimbali kutoka duka la Beauty Haven wakiwa kwenye banda lao wakati wa Tamasha la Po Up Bongo.
Tanya akiwa na wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye Pop Up shop
Atu Mynah akimtaja mshindi wa bahati nasibu siku hiyo
Kutokea banda la Beauty Heaven kulikuwa na bidhaa mbalimbali pia
Natasha akizungumza na mmoja kati ya washiriki waliojitokeza kuonesha bidhaa siku hiyo.

Na Mwandishi Wetu
ONESHO la mauzo ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wabunifu wa hapa nchini, Pop Up Bongo lilifanyika hivi karibuni na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Mratibu wa onesho hilo lililofanyikia Trinity Oysterbay, Natasha Stambuli alisema kuwa zaidi ya wajasiriamali 15 walijiotokeza kuonesha na kuuza bidhaa zao.

Alisema kuwa bidhaa mbalimbali kama vile nguo, vito, viatu na vinginevyo viliuzwa na wajasiriamali hao walipata wasaa wa kuongeza wigo wao kibiashara kwa kukutana na wanunuzi.

“Pop Up Bongo inalenga kuwaweka karibu zaidi wajasiriamali na wanunuzi kwa kuwakutanisha mahala hapa na kisha hata wakishafanya mauzo wanakuwa na wasaa wa kuonana hata baada ya tamasha hili na kuendeleza uhusiano wa kibiashara,” alisema Natasha.

Pia ametoa wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kuhudhuria maonesho mbalimbali ya biashara ili kupanua wigo zaidi wa ufahamu wa aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo nchini.

Natasha alisema kuwa kwa kutembelea maonesho hayo watapata wasaa wa kufahamu aina mbalimbali za bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara mbalimbali na kujua ni wapi pa kwenda kujipatia mahitaji.

Alisema kuwa Pop Up Bongo ikiwa chini ya udhamini wa kinywaji cha Smirnoff inalenga kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa bidhaa mbalimbali zitengenezwazo hapa nchini na wanunuzi kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali wa hapa nchini kuongeza pia wigo wa biashara zao.

Kwa upande wake, Meneja Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija, akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa kampuni hiyo inatambua nafasi ya wajasiriamali katika kuendeleza uchumi wa nchi na ndiyo maana imeamua kuunga mkono Pop Up Bongo.

“SBL kwa kupitia kinywaji chetu cha Smirnoff tumeamua kudhamini Pop Up Bongo kwa kuwa ni mahala pazuri kwa wapenzi wa kinywaji hiki kukutana huku wakijipatia mahitaji yao kadhaa kutoka kwa wauzaji wanaouza bidhaa zao katika Pop Up Bongo,” alisema Shomari.

No comments: