Tuesday, December 29, 2015

Papaa Msofe, Alex Massawe Wahukumiwa...Mke wa Marehemu Aangua Kilio cha Furaha Baada ya Haki Kutetendeka


Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, imetoa hukumu kwa mfanyabiashara Marijani Abubakar, almaarufu Papaa Msofe, Alex Massawe na Makongoro Nyerere kwa kosa la kughushi hati ya umiliki wa nyumba iliyopo Mikocheni jijini Dar, mali ya marehemu Onesphory Kituly aliyeuawa kwa kupigwa risasi na majambazi mwaka 2011.
Kesi hiyo iliyonguruma kwa takribani miaka saba tangu 2007, ilifikia tamati Desemba 22, mwaka huu na kuwakuta na hatia washtakiwa hao baada ya upande wa utetezi kushindwa kuwasilisha vielelezo vinavyowapa uhalali wa kumiliki nyumba hiyo.
AlexMassaweAlex Massawe.

Akisoma hukumu hiyo, jaji wa mahakama hiyo, John Nchimbi mbele ya wakili wa Msofe na wenzake, Majura Maghafu alisema kuwa baada ya kupitia hoja zilizowasilishwa na pande zote mbili, mahakama imeamua kumtangaza mke wa marehemu Onesphory, Mary Kituly kuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo.
“Pia mahakama imewatoza fani ya shilingi milioni 300, Papaa Msofe, Massawe na Nyerere pamoja na asilimia 12 ya fedha hizo kama fidia ya gharama za uendeshwaji wa kesi hiyo,” alisema Jaji Nchimbi.

Mara baada ya kusomwa hukumu hiyo, mke wa marehemu, Mary aliangua kilio cha furaha na nduguze mbele ya jaji baada ya kuona haki imetendeka, kitu ambacho hakuwa akikitarajia.

“Yaani siamini macho yangu, maana jinsi kesi ilivyonisumbua kwa miaka saba, nimefarijika sana kwa haki kutendeka maana nilikuwa nikishindana na watu wenye pesa, damu ya mume wangu haijapotea bure, namshukuru Mungu kwa kweli,” alisema Mary alipokuwa akizungumza na waandishi wetu ambapo alimshukuru pia Rais John Magufuli kwani serikali yake inajali haki.
Msofe na wenzake walifunguliwa kesi katika mahakama hiyo mwaka 2007 baada ya kudaiwa kughushi hati ya nyumba kwa kuhamisha umiliki wa nyumba namba 288 iliyopo Mikocheni, Dar iliyokuwa ya marehemu Kituly na kuweka jina lake kisha kumuuzia Masawe kinyume cha sheria.
Ilidaiwa kuwa kabla ya kufariki dunia, marehemu Kituly alimkopa shilingi milioni 30 Msofe kwa dhamana ya hati ya nyumba hiyo kwa makubaliano ya kumrudishia kiasi hicho kwa muda wa miezi sita.

Inadaiwa kuwa baada ya miezi mitano, marehemu alipata kiasi hicho cha fedha na kurudisha kwa Msofe na kutaka hati yake, lakini alianza kuzungushwa kuanzia kipindi hicho hadi alipokufa kwa kuuawa na watu wasiojulikana mwaka 2011.

Oktoba 30, 2007, Msofe aliwatoa kwa nguvu marehemu, mke wake na watoto kwa madai kuwa nyumba hiyo imeuzwa kwa Massawe.

7 comments:

Anonymous said...

i hate to say this: hapa bongo nimeshuhudia udhulumati wa mali za watu kutoka kwa wachaga zaidi ya kabila lingine lolote. I know it is very sensitive thing and I may sound tribal but this is fact and I can prove it. I stand to be corrected.

Anonymous said...

Wewe mporipori Papa Msofe na Makongoro Nyerere sio wachaga kwa hivyo tukome kabisa mkabila mkubwa wee

Anonymous said...

What about kesi ya kuua?? Au ndio basi? Don't you see washitakiwa wanahusika na kifo cha mume wa huyo mama??

Unknown said...

Mwandishi mbona hujatuhabarisha vizuri kuhusu hukumu waliyopata watuhumiwa?

Anonymous said...

Mdau wa December 29, 2015 at 9:17 PM - Nafahamu sensitivity ya mtazamo wangu lkn naamini ninachokisema. Umeona kesi mpya ya makontena 11,884? Hivi unajua wengi wao mle ni wachaga? Not only that, kuna matukio mengi ya wizi/dhuluma/ujambazi na wahusika ni watu unaowatetea lkn nawafahamu. Nina factual evidences to prove what I am saying.

Jamaa zako ni sehemu ya jamii yetu na maongezi yangu ni informal type of sanction. I will be more than happy to have a debate with you on this issue.

Anonymous said...

HUYO PAPA MSOFE NI MCHAGA WA DAMU NANI ASIEJUA KABILA LAKE NA HUYO MAKONGORO NYERER NI MCHAGA TAPELI WA JINA HILO MPAKA LIMEKUBALIKA WOTE NI SWAIN WACHAGA KAMA KINA LOWASSA,UKIMPANGISHA NYUMBA YAKO LAZPMA ALETE UJANJA, WA KUTAKA KUKUDHULUMU.

Anonymous said...

Heri mimi sijasema. Kuna mambo ya kishenzi nimeshuhudia wachaga wakifanya hata siamini macho yangu. Kule uchagani ukiwa mwizi ndiyo unaonekana mjanja. What a shame?