Tuesday, December 29, 2015

SAMATA AZUNGUMZIA USAJILI WAKE KUTOKA AFRICA LION KWENDA SIMBA


DAUDA TV: HII NDIYO SAFARI NDEFU YA SAMATTA KUTOKA MBAGALA KWENDA ULAYA, HAPA AELEZA ALIVYOSAJILIWA NA SIMBA KUTOKA AFRICAN LYON


Mbwana Samatta ‘Popa’ au waweza kumwita ‘Eto’o wa Mbagala’ jina hili limezidi kupata umaarufu kila kukicha kwenye medani ya soka si Tanzania pekee bali Afrika na sasa limesha vuka mipaka ya Afrika na kuenea duniani kote.
Mchezaji huyu alianza kupata umaarufu wakati anakipiga kwenye klabu yake ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam ambapo alifanya vitu ambavyo viliishaishi klabu ya Simba SC imsajili kutoka African Lyon.

Samatta anaelezea mwenyewe safari yake ya soka ilivyoanza kutoka African Lyon kwenda Simba, alikuaje alikutana na nani pamoja na changamoto ambazo alikutana nazo na ni namna gani aliweza kuzivuka hadi kufikia mafanikio aliyonayo mpaka sasa.

Ungana na shaffihdauda.co.tz upate kujua maisha ya Samatta ndani na nje katika safari yake ya kutoka Mbagala kuelekea bara la Ulaya, amepita njia zipi na nini malengo yake ya baadae katika soka.

Wakati natoka African Lyon kwenda Simba hata viongozi wa Simba waliokuwa wanashughulikia sualala usajili walikuwa wananichukulia kama mchezaji mdogo ambaye nahitaji muda wa miaka miwili au mitatu kabla sijaanza ku-perform

Simba ilikuwa ni timu ambayo imejaza nafasi lakini wanaona huyu ni mchezaji mzuri kwahiyo wakaamua kunichukua ili baada ya muda flani niwasaidie kwasababu walikuwa hawana uhakika kama wachezaji waliokuwanao wangeendelea kuwepo.

Walikuwa hawajanichukulia kama mchezaji mkubwa ambaye watamtumia moja kwa moja ndiyomaana zikatokea hata changamoto nyingine kwenye masuala ya mkataba.

Angalia viedeo samatta akielezea safari yake ilivyoanza kutoka African Lyon kwenda kwa wekundu wa Msimbazi Simba. Credit:ShaffihDauda

No comments: