Tuesday, December 8, 2015

TANESCo walivyokatisha nyumbani kwa Wema Sepetu, kilichofatia ni hiki hapa.. na Idris yumo ??


Oparesheni ya TANESCO kukagua nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa imeendelea kama ambavyo kumekuwa na story kwenye vyombo vya habari !! Story imegusa mitandaoni, ikamfikia Soudy Brown… leo akaanza na kiongozi wa TANESCO, jamaa amesema walifika wakagundua kuna tatizo kwenye mfumo wa mita ya LUKU nyumbani kwa Wema, walipohitaji maelezo ya wanaoishi kwenye nyumba hiyo, Wema hakuwepo na badala yake akatokea Idris. Soudy Brown akageuka kumcheki Idris… Idris amesema alikuwa anapita kwenda kwenye mishemishe zake ndio akakutana na ishu hiyo ya TANESCO nyumbani kwa Wema, ila hajui chochote kinachoendelea kwa sababu haishi na Wema kwenye nyumba hiyo.

Audio link ya kilichotokea: http://hu.lk/6p67z780sa68


-Millardayo.com

http://millardayo.com/uheard0812/

1 comment:

Anonymous said...

Mama ongea na Tanesco