Saturday, December 5, 2015

TANZANIA DAY IN SEATTLE, WA


TANZANIA COMMUNITY OF SEATTLE, WASHINGTON 

Ndugu Watanzania mwenzangu,


Jumuiya yenu ya Tanzaseattle imekamilisha matayarisho ya kusherehekea Siku ya Mtanzania. Hii ni miongoni mwa Sherehe za mwaka ambazo husherehekewa na Jumuiya.

Njoo ufurahi pamoja na kukutana na wanadiaspora kutoka nchi mbali mbali. 

Sherehe hii ni ya kujivunia Utanzania na Uafrika wako kwa kivazi na burudani mbali mbali. 
Sherehe hii itaambatana na maonesho ya mavazi ya Kitanzania kutoka kwa Mwanamitindo maarufu Duniani:  Asia Idarous Khamsin kutoka Tanzania.
Njoo ujipatie ladha ya Chakula safi cha Kitanzania pamoja na kucheza muziki wa asili ya  Kitanzania ukianawirishwa na muziki wa Dansi( Mlimani Paki, Marijani Rajabui n.k bila kusahau nyimbo mwanana za Taarab kutoka visiwa vya Zanzibar)
Jumuiya inakuomba uvae nguo ya Kitamaduni (optional). Pia mutaweza kununua nguo kwenye maonesho ya mavazi siku hiyo hiyo.

Pahala ni:

411 156th Ave NE
Bellevue, Wa 98007

Mlango kuanza  kufunguliwa Saa Moja usiku (7pm) - Ratiba kamili itakuwepo siku ya shughuli hii kwa matukio tofauti mbali mbali yakufurahusha.


Kingilio ni Dola 10 kwa mtu. ($10 per person)

Tafadhali mjulishe rafiki na jirani yako.


Karibuni nyote kwa wingi,


Uongozi wa TanzaSeattle, Seattle Washington USA.
Taarifa hii imetolewa na Mayor of Seattle (A.Dola) 

No comments: