Saturday, December 5, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE, KWENYE MKUTANO WA TANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati walipokutana kwenye Mkutano wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, wakati wakitembelea Mabanda ya maonesho ya mkutano huo uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana Dec 4, 2015. ambapo Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo . Picha Zote na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing (kushoto) wakati walipokutana kwenye Mkutano wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, walipokuwa wakitembelea Mabanda ya maonesho ya mkutano huo uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana Dec 4, 2015. ambapo Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, na Rais Mstaafu wa awamu ya Tano, Dkt. Jakaya Kikwete, wakiangalia moja ya Ndege ya Kivita ya mfano, wakati walipotembelea Mabanda ya maonesho ya Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana Dec 4, 2015. Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan, akiongozana na Rais Mstaafu wa awamu ya Tano, Dkt. Jakaya Kikwete, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing, wakiangalia moja ya Ndege ya Kivita ya mfano, wakati walipotembelea Mabanda ya maonesho ya Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliofanyika Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana Dec 4, 2015. Dkt. Jakaya Kikwete alihudhuria mkutano huo kama Rais Mstaafu mwalikwa. Mkutano huo unamalizika leo.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Makamu wa Rais wa Sudan, Mhe. Bakri Hassan Salih, walipokutana na kwenye mkutano wa mwisho wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini, ambapo Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, pia alihutubia.\
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Rutageruka Mulamula, kabla ya kuhutubia katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipitia 'Document' kabla ya kuhutubia katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipitia 'Document' kabla ya kuhutubia katika Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika ukumbi wa mkutano wakati akijiandaa kuhutubia kwenye Mkutano mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, unaomalizika leo jijini Johannesburg Afrika ya Kusini. 

5 comments:

Anonymous said...

maelezo haya yamekuzwa sana na lengo hapa linaonekana kua ni moja tuu,kumpandisha chart rais mstaafu jmkikwete[ambayo kwa madudu na uhujumu kwa yanayofumuliwa sasa na mhe.rais jpmagufuli]jmkikwete hastahili sifa yeyote kwanza kwa sasa.nauliza gharama hizi za mhe.kikwete kuhudhuria kikao hiki amelipiwa na nani?na ujumbe wake ulihusisha maafisa wangapi wanaoendelea kulipwa na serikali?rais wetu hakushiriki 'tamasha lile la kichina'kwa kutahadhari gharama isiyoambatana na tija yeyote akamtuma makamu wake mhe.samia suluhu.ni dhahiri serikali imeokoa mabillion.nchi kiuchumi,ilikwisha haribika.kashfa ya makontena,safari na semina hewa,TRA,kitengo cha lishe ya rais,coco beach kuuzwa kwa yusuph manji,wizara 32,ulaji taasisAi ya bunge,muhimbili[YOTE HAYA NDANI YA SIKU 30 SERIKALI MPYA]

Anonymous said...

Uhusiano WA Tanzania na China unatia shaka
Kwanini kika kukicha wanakamatwa wachina na meno ya tembo , faru
Jamani kulikoni
Tuoene aibu viongozi hasa mnapotoa mapicha na viongozi wa China

Anonymous said...

Huyu JK anaharibu legacy yake kama rais mstaafu haijalishi kama safari haigharamiwi na serikali lakini kwa kipindi hiki angetoka kwenye picha ya waTZ kwa makubwa yanayofanywa na JPM katika siku 30, pia mkuu wa nchi amesema hakuna safari za nje wewe kutwa uko nje inaonyesha kutokuwa na nidhani kwa mkuu wa nchi ingawa umestaafu lakini ni bado sehemu ya serikali, busara inabidi kupewa kipao mbele hapa.

Anonymous said...

Why huyu Kikwete hapa? Bado anaendelea kutumbua tu hela za walalahoi watanzania nae amesha staff. Huyu baba si bure anaagenda huyu na hawa wachina. Yatamshinda hili ni Taifa

Anonymous said...

Wapiga Picha na ikulu
Picha zingine kulikoni
But we love it it's show the reality of our leaders loop
Shame CCM
Magufuli Huna watu