Tanzania inatarajia
kurudishiwa dola za kimarekani milioni sita sawa na shilingi za kitanzania
bilioni 14 zilizotozwa isivyostahili na benki ya Stanbic Tanzania kupitia
kampuni ya EGMA.
Fedha hizo
zinarejeshwa kwa Tanzania baada ya benki ya Stanbic Tanzania kupitia kampuni ya
EGMA kuongeza asilimia moja ya riba baada ya serikali kukopa dola milioni mia
sita kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo mwaka 2012 na 2013
na kutakiwa kuzilipa katika kipindi cha miaka 7 kwa riba ya aslimia 1 nukta nne
na badala yake ikatozwa asilimia mbili nukta nne ya mkopo wote hali iliyotokana
na benki kuu kubaini baadhi ya matatizo.
Kwa mujibu wa Balozi
Ombeni Sefue udanganyifu wa utaratibu wa kumtafuta wakala wa ndani yaani Local
Agent uliofanywa na benki ya Stanbic Tanzania ulibainika kutokana na uchunguzi
uliofanywa na kampuni ya Serious Fraud Office ya London na kufungua kesi ambayo
kampuni hiyo ilipata ushindi November 30, 2015 na kuiwezesha Tanzania
kurejeshwa fedha hizo huku Balozi Sefue akieleza hatua zinazochukuliwa ndani ya
Tanzania kuhusiana na kampuni ya EGMA na benki ya Stanbic Tanzania.
Aidha Balozi Sefue
ameishukuru serikali ya uingereza kwa ushirikiano na kuyataka mataifa mengine
ya Ulaya kuzisaidia nchi zinazoendelea kupambana na rushwa kutokana na ulaghai
unaofanywa na makampuni ya nchi za ulaya badala ya kuzinyooshea vidole kuwa
zimeshindwa kupambana na rushwa.
CHANZO: ITV TANZANIA
1 comment:
Zikasaidie hospitali za mikoa watu mikoani tusisahaulike
Post a Comment