ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, December 20, 2015

TAWI LA CCM NEW YORK WAKUTANA NA KUONGELEA MAENDELEO YA TAWI LAO NA KUTUMA PONGEZI KWA RAIS WA WAMU YA 5 DKT MAGUFULI.

Hapa ni meza kuu mwenyekiti wa tawi Seif Akida akiwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi kama mgeni rasmi. Viongozi wa Tawi la CCM New York walikutana na Watanzania kuzungumzia maendeleo ya tawi na pia kujipongeza kwa CCM kutoa Rais mwingine kuongoza Tanzania kwa awamu ya 5. Rais huyo ni Dkt Pombe Magufuli  ni Rais mteule kutoka chama tawala CCM na toka aingia madarakani ameshajijengea heshima kutokana na utendaji kazi wake wenye kauli mbiu ya 
#HAPA KAZI TU.#
Mh. Balozi akipata ukodak na viongozi wa tawi kama ukumbusho ukumbini hapo picha zingine za balozi na Watanzania nenda soma zaidi.

4 comments:

Anonymous said...

Hawa ndo wasiolipa kodi mizigo Yao
Fyuuuuuuuu
Kwani Tanzania kuna ofisi za public or demokrasi. Party

Anonymous said...

Na sis Republic Party tawi la Bungoni kwa Malap, tutakuwa na mkutano wetu wa kesho kesho asubuhi saa mbili.

Anonymous said...

Tafuteni kazi mfanye kama ccm inamaana msingekuwa hapa mlipo

Anicetus said...

New York Tanznain Commnunity wajipanga na uchaguzi wa kupata viongozi january 2016; Tawi la CCM New York wakutana na Kuongelea maendeleo ya Tawi lao na kutuma pongezi kwa raisi wa awamu ya tano. Ukianagalia hapo wanachama ni wale wale na wananfanya kazi zao, ni wachapa kazi na wanajitegemea kuboresha maisaho yao na watanzania kwa ujumla. Kukutana kwao ni social event ammbayo inaunganisha watanzania bila kubagua mtu yeyote na ubalozi wa Tanzania unashiriki kuboresha watanzania wawe pamoja na washirikiane kwa mamabo yote yanayohusi jammii na maendleleo ya kuitangaza sifa za Tanzania huku ugaibuni.