ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 17, 2015

WALIOJENGA PEMBEZONI YA BONDE LA MTO MSIMBAZI WAPITIWA NA BOMOA BOMOA

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Manispaa za jiji la Dar es salaam zitafanya zoezi la kuondoa wavamizi maeneo yote ya Mabondeni, kingo za mito  na za Bahari, maeneo ya wazi, maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi zaidi ya 150 katika  jiji la Dar es salaam. Bomoa bomoa ya leo inaendelea katika Bonde la mto msimbazi.Mkuu wa Kitengo cha Sheria Balaza la Taifa la usimamizi wa mazingira Tanzania (NEMC), Manchale Heche akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Bomoabomoa maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi nakuwataka wananchi waliojenga katika fukwe za bahari Kingo za mito na mikondo ya bahari kuhamisha mali zao mapema.
Wananchi wakitoa samani pamoja na vitu mbalimbali ndani ya nyumba zao ili kupisha ubomoaji wa nyumba zilizo maeneo hatarishi. 
Ubomoaji ukiendelea maeneo ya Mto msimbazi jijini Dar es Salaam. 
Wananchi pamoja na polisi (Wazee wa kazi) wakiangalia ubomoaji unavyoendelea bila vurugu.
Vijana wakiokota vitu mbalimbali katika maeneo yaliyobomolewa leo jijini Dar es Salaam. 

Wananchi wakiwa maeneo hatarishi ambayo yanasubiri kubomorewa. 
Uondoaji wa vyuma katika nyumba inayongoja kubomolewa. 

 Wazee wa kazi wakihakikisha usalama wa eneo ya ubomoaji. 
 Vitu mbalimbali vikiwa vimetolewa nje ili kupisha ubomoaji wa nyumba.

3 comments:

Anonymous said...

Kwa nini hawa watu walipewa huduma za umeme na wangine mpaka kupata huduma nyingine za maji. Hii maana yake na watumishi wa serikali wanahusika au walihusika. Basi baada ya kubomoa wafanyakazi waliohusika nao wasimamishwe kazi.

Jay said...

Hii safi sana kwa serikali na manispaa ya jiji la Dar kuwa serious na hawa watu kwani wanaharibu sana mazingira. Wengi walishaonywa kutojenga ama kuishi mabondeni ila walifanya mdhaha kwa sababu hatukuwa na rais then, ila sasa mwendo mdundo. Tanzania hii ya sasa lazima ibadilike tu na raia wake wabadilike.

Anonymous said...

PONGEZI SERIKALI KWA KUONDOA UCHAFU HUU KWENYE MITO NA MABONDE YETU. HATA KAMA WALIOMBA NA KUPEWA VIBALI VYA KUJENGA, WALISHINDWA KUTUMIA AKILI KUJUA HAPO NI KARIBU NA MITO NA PIA NI MABONDENI HIVYO WANGEJENGA WANGEHATARISHA MAISHA YAO??? SERIKALI ANGALAU INAFANYA KAZI SASA.