Huo ndio uchafu uliotupwa katika kijiji cha shenda siku ya tarehe 9 Disemba ambapo ilikuwa siku ya usafi kwa nchi nzima
Wanakijiji wa kijiji cha Shenda wilayani Geita wakiongea na waandishi wa habari waliotembelea kijiji hicho ambapo walilalamikia kutupwa kwa takataka katika kijiji hicho siku ya tarehe 9 ambapo ilikuwa siku ya usafi kwa nchi nzima
Krantz Mwantepele,Geita
Wananchi wa kijiji cha Shenda katika kata ya Masumbwe wilayani Mbogwe mkoani Geita Wameitaka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Mbogwe kuziondoa takataka zilizowekwa kijijini kwao kufuatia zoezi la usafi la December 9 Lililofanyika nchi nzima.
Wakiongea na waandishi wa habari za mtandaoni wananchi hao wanakijiji hao wamesema kuwa wanashangazwa na kitendo cha halmashauri ya wilaya kutupa takataka katika kijiji chao licha ya kwamba hakuna dampo la uchafu eneo hilo.
Wameongeza kuwa taka hizo ni hatari kwa afya zao kwani zimetupwa karibu na eneo la shule ya msingi,Makazi ya watu na vibanda vya mama ntilie hali inayozua hofu ya kuzuka kwa magonjwa ya mripuko kwani taka hizo zimeanza kuoza na kusambaa katika makazi ya watu kipindi hiki cha masika.
Sambamba na hayo wameshangazwa na maamuzi ya ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri kutupa taka hizo katika kijiji chao licha ya kuwa yapo maeneo mengi ya wazi ambayo yangeweza kutumika kutupa taka hizo ambazo kwa sasa zimekuwa kero katika kijiji chao hasa kutoa harufu mbaya na funza.
Kwa mujibu wa kaimu mtendaji wa kijiji cha Shenda Joseph Jaseda amesema sehemu zilizotupwa taka hizo ni makazi ya watu na kwamba walipouliza kuhusu hatua hiyo waliambiwa kuwa gari la kuzoa taka liliharibika sehemu hiyo na ndipo walipoamua kutupa taka hizo.
Kwa upande wake afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe…………..amesema kuwa baada ya wananchi kulalamika walienda kuweka dawa ya kuwa wadudu katika taka hizo na kwamba hawajaziamisha kutokana na taka hizo kutokuwa na madhara kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment