Tuesday, January 12, 2016

BREAKING NEWS: SIMBA YAMTIMUA KOCHA WAKE DYLAN KERR

Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba inawaarifu umma kupitia vyombo vya habari.uamuzi wake wa kuvunja mikataba yake na makocha wake  - kocha mkuu Dylan Kerr kutoka uingereza na kocha wake wa makipa Iddi Salim.

Katika uamuzi wake uliofanywa mchana huu na kikao cha kamati ya utendaji, ambapo makocha hao waliitwa, klabu ya Simba na walimu hao kwa pamoja wamekubaliana kuvunja mikataba ya ajira zao kwa faida ya pande zote mbili.
Kwa sasa kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja atakuwa na timu.huku mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.
Mwisho uongozi unawashukuru walimu hao kwa huduma waliyoitoa katika kipindi chote cha uwepo wao klabuni.



Imetolewa na Haji S.Manara

Mkuu wa mawasiliano wa klabu ya Simba.
Simba nguvu moja

No comments: