Monday, January 18, 2016

BREAKING NEWS: WANANCHI WA BONDE LA MKWAJUNI WAFUNGA BARABARA NA KUFANYA FUJO

Hali si shwari hivi sasa katika eneo la Bonde la Mkwajuni Kinondoni jijini Dar es salaam, na inaelezwa kuwa baadhi ya Wananchi wamechoma mataili pande zote za barabara na hakuna gari kupita. Jeshi la Polisi lipo eneo la tukio hivi sasa kukabiliana na tukio hilo ambalo chanzo chake unadaiwa ni baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa walikuwa wakazi wa eneo lililobomolewa ambao wameingia barabarani na kufanya fujo. Pia gari la zimamoto limefika eneo la tukio ili kuzima moto huo. (Picha na Henry Mdimu na Yasin Ngitu)
Akizungumza mmoja kati ya waathirika wa bomoa bomoa hiyo, Bi Fatuma Said, amesema wanashindwa kuondoka katika eneo hilo kwa kuwa hawana sehemu ya kwenda huku akiitaka serikali kuwafikiria.

“Sio kwamba tumegoma kuondoka wengine sisi hatuna sehemu ya kwenda,” alisema. “Sisi baada ya kubomolewa nyumba yetu tukashindwa kuondoka kwa kukosa pa kwenda.Tukaamua kujenga hapa vijibanda ili serikali itufikirie lakini tunashangaa leo asubuhi vibanda vyetu vimewekwa X kwamba wanataka kubomoa. 
Saa tano tumeingiliwa kwenye vibanda vyetu sisi tukakimbia wao wakachoma ndio baadhi ya wananchi wakaingiwa na hasira na kwenda kuchoma matairi barabarani,”alieleza.
Hata hivyo mtandao huu ulijaribu kuzungumza na afisa wa polisi aliyekuwepo katika eneo hilo, lakini alisema watatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo. Hadi sasa polisi wanawashikilia vijana kadhaa wanaohusishwa na tukio hilo.

No comments: