Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,Mh.Mwigulu Lameck Nchemba akisikiliza kero za wadau wa machinjio ya Vingunguti usiku huu wa January 1/01/2016.Mwigulu Nchemba akishuhudia Ng'ombe aliyetayari kwa taratibu za kuchinjwa kwaajili ya kitoweo.
Mbuzi wakiwa tayari kwaajili ya kuchinjwa kwenye machinjio hayo ya Vingunguti.Mbuzi hawa asilimia kubwa wanatoka mnada wa pugu ambao Ushuru wake unakusanywa na serikali kuu.Waziri Mwigulu Nchemba akikagua maeneo ya machinjio hayo usiku huu.
Mwigulu Nchemba akitoa maagizo kwa uongozi wa Machinjio ya Vingunguti kukutana kesho saa 2:00 asubuhi kwa wahusika wote wenye dhamana na Machinjio hayo,Mkutano utafanyika eneo la Machinjio hayo.
Katika hatua ya kushitukiza,Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba amefanya ukaguzi wa Machinjio ya Vingunguti usiku huu.
Mh.Mwigulu Nchemba amefika kwenye Machinjio hayo usiku huu ilikushuhudia Mifugo ikiandaliwa kwaajili ya kitoweo cha wananchi.Uchinjaji wa Ng'ombe na Mbuzi katika machinjio haya hufanyika nyakati za Usiku kuanzia saa 4 hadi 10 alfajiri.
Mbali na kusikiliza kero na maoni ya wananchi kuhusu uendeshwaji wa Machinjio hayo,Mwigulu Nchemba ameshuhudia utafunwaji wa kodi ya serikali inayokusanywa kwenye mnada wa pugu.
Utafunwaji huo unatokana na uandikaji wa kibali cha mifugo michache kuja Machinjioni ili hali mifugo Zaidi huingizwa machinjioni bila kibali.Matharani hii leo Mh.Waziri ameshuhudia Ng'ombe waliotoka mnada wa pugu ambao wameshalipiwa kodi wakiwa 1450 lakini kibali chake kimeandikwa Ng'ombe 300 tu.Inamana kuna ng'ombe 1150 wamelipiwa ushuru lakini machinjioni kimeletwa kibali cha ng'ombe 300 wakati kwa kuwahesabu ng'ombe hao wanazidi 1000.
Kutokana na hali hiyo,Mh.Waziri ameagiza wahusika wote kufika kesho kwenye mkutano wa asubuhi kwaajili ya hatua stahiki kuchukuliwa,Mwigulu amesisitiza kuwa kwa mtu yeyote mwenye dhamana na kusimamia sekta ya kilimo,Mifugo na Uvuvi afanya kwa mujibu wa sharia,vinginevyo hakutakuwa na huruma kwa wanaohujumu.
5 comments:
Ukiachia mbali upotevu wa kodi ya serikali, process nzima kuanzia kwenye machingiyo mpaka kwenye mabucha ni jipu linalohitaji tiba ASAP.
Ukitaka kufahamu kiwanda cha kuzalisha kipindupindu basi fatilia process ya utaarishaji,na uujazi wa nyama nchini. Kuna haja ya wizara 3 (mifugo,Afya & makamu wa raisi- mazingira) kufanyakazi kwa kushirikiana kuhakikisha kuwa afya ya mlaji inazingatiwa wakati wote.
Mabucha & machinjio yetu ni machafu
Nzii,paka & mbwa hawatakiwi katika maeneo hayo...
Tatizo Wabongo mnapenda na mnapumbazwa sana kwa mambo madogo yasiyokuwa na tija kwa Taifa. Hivi zile siku saba za kulipa kodi wa zile kontena zimeishia wapi na nini kimefanyika mpaka sasa?
kwani Ng'ombe moja ushuru kiasi gani. minada na machinjio duni kumbe kuna majizi yanatafuna 80% ya kodi.
Adhabu kwa mkwepa kodi ni ndogo sana ndio sababu wataendelea bila uoga. Mabadiliko ya sheria ni lazima ili kokomesha ukwepaji kodi.
Kama serekali imeamua kutangaza vita kwa wakwepa kodi waonyeshe nia kwa vitendo sio ambushi inayofanywa na mawaziri.
Hii nchi ina vyanzo vingi kweli vya mapato. Sometimes unashangaa tunashindwaje kumudu huduma ndogo tu kama maji safi na salama kwa wananchi.
vinchi vidogo kama Rwanda na Botswana ambazo hazina rasilimali zozote kubwa nchini mwao zikipaa mno kiuchumi?
Usanii tuu huu alivyokuwa waziri wa fedha amesahau yeye alikuwa anafanya nini kwenye invoice wakati wa uagizaji ya gari kutoka japan.
dj luke usibaniye comment tafadhali mkuu
Kwanza watake radhi watanzania kwa maneno yako,vilex2 kama siku 7 za makontena ndio principle issue kwako basi nivema ukafuatia taarifa hizo TRA au wizara ya fedha.
Kwa ujumla watanzania wengi bila kujali itikadi za vyama vyetu tunaunga mkono jitihada zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya 5 katika kupambana na wahujumu uchumi,wazembe n.k.
Si rahisi kuona matokeo chanya ya juhudi hizi ndani ya miezi 3,kwani vita ya kupambana na mfumo mbovu na ku change mindsets za watu kama wewe hakika si nyepesi.
GOD BLESS TANZANIA.
Sasa unachombishia huyu bwana/bibi sikioni. Unakubali kwamba mfumo mbaua, yeye kauliza matokeo ya siku saba za kodi yako wapi? Au hii ni sawa na kucheza mira uwanja mzima bila kufunga goli lakini unataka tukushangilie? Idiot!
Post a Comment