Baraza kuu la uongozi la taifa la chama cha wananchi CUF, kwa kauli moja limeridhia kutokushiriki uchaguzi mkuu wa Zanzibar huku likisisitiza kuwa mamauzi ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Oct 25 mwaka jana yalikuwa batili.
Mapema jan 28, baada ya baraza kuu la uongozi la CUF kutumia saa 4, kujadili agenda moja tu ya kushiriki au kutokushiriki katika uchaguzi wa mach 20 mwaka huu, makamo mwenyekiti wa CUF taifa akatanagza maadhimio kadhaa ya kikao hicho.
Miongoni mwa maazimio hayo 12 ya kikao hicho ni pamoja na ukiukwaji wa katiba ya Zanzibar na sheria ya uchaguzi namba 11 ya mwaka1984, huku katibu mkuu wa CUF akishutumu kile alichokiita ni mbinu chafu za kuchafua daktari la wapiga kura mjini Zanzibar.
Aidha tamko hilo limezitaja jumuiya za SADC, EAC, AU, umoja wa Ulaya, jumuiya ya madola na nchi za Uingereza na Marekani ambazo amezitaja kuunga mkono uchaguzi wa Oct 25 mwaka jana, huku likiitaka serikali kutaafkari upya uamuzi wake wa kuitisha uchaguzi mpya mwezi march.
Haya yanajili baada ya tamko la mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha kutangaza kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar mapema Oct 28, huku tarehe ya uchaguzi huo wa marudio ikitajwa kufanyika mapema march 20 mwaka huu.
2 comments:
Mpeni maalimu seif
Haki yake jamani dunia iwe na amani!
Mpeni maalimu seif
Haki yake jamani dunia iwe na amani!
Post a Comment