ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 28, 2016

SERIKALI YATANGAZA KUFILISIWA KWA MAFISADI NA WAHUJUMU UCHUMI

Mkurugezni wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani)
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, (DPP), Bw. Biswalo Mganga, (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari ambao ulimkutanisha yeye, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kutoka jeshi la polisi, (DCI), Kamishna wa polisi, Diwani Athumani, (kushoto), na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), Bw.Alex Mfungo, kwenye makao makuu ya polisi jijiniDar es Salaam, Januari 28, 2016. Katika taarifayao ya pamoja, taasisihizo zimeanza kutaifisha mali za watuhumiwa wa Ufisadi na Uhujumu uchumi na kuwataka wananchi kujitokeza kuwataja watuhumiwa wanaomiliki mali hizo kokote waliko.(Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
DCI Kamishna wa Polisi Diwani Athumani akizumza na waandishi wa habari leo.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo
Kamishna Diwani Athumani akizungumza
Bw. Mfungo, (kulia), akiwa na DPP, Mganga
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waandishi wa habari wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na watatu hao
Mmiliki wa Blog ya Full Shangwe, John Bukuku akiuliza swali.
Bw. Oliver Stolpe, (kushoto) kutoka UNODC ambao ni wadau wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka DPP, akiwa na Mkuu wa Mahusiano Ofisi ya DPP, Bw. Oswald Tibabyekonya wakitoka kwenye mkutano huo

1 comment:

Anonymous said...

Komba kila kitu. Waachie tu nguo walizovaa, wezi na wabinafsi