Wakati watu mbalimbali wakimminia sifa Rais John Magufuli kwa kubana matumizi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga amesema uwingi wa makatibu wakuu unakinzana na dhana ya yake ya kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri.
Dk Mahanga alikuwa Naibu Waziri wa Lazi na Ajira tangu mwaka 2008 na hakuwahi kuhamishwa wala kupandishwa hadi ngazi ya uwaziri hadi Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ilipomaliza muda wake na baadaye kujiunga na Chadema.
Katika waraka wake alioutoa kwenye mitandao ya kijamii, Dk Mahanga alimkosoa Rais Magufuli akisema ameongeza ukubwa wa Baraza la Mawaziri baada ya kuteua makatibu wakuu 27 wakati anawaaminisha wananchi kwamba wizara ni 15 tu.
Dk Magufuli ameunda baraza lenye mawaziri 15, na manaibu waziri 19 na hivyo kufanya baraza lake kuwa na jumla ya mawaziri 34, tofauti na baraza lililopita lililokuwa na mawaziri 55.
Uamuzi wa kupunguza idadi ya wizara ulikumbana na changamoto ya nafasi za makatibu, ambao hata hivyo baadhi amewarudisha wizarani ambako watapangiwa kazi na kubakiwa na makatibu 27.
“Si kweli kwamba kapunguza ukubwa wa Serikali, bali kaongeza ukubwa wake. Sina hakika kama wasaidizi wa Rais wamemshauri na kumweleza kwamba wizara si ofisi ya waziri bali wizara ni ofisi ya katibu mkuu,” alisema Dk Mahanga akifafanua kuwa katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu wa wizara na afisa masuhuli.
Alisema katibu mkuu ndiye mwenye dhamana ya utendaji na ndiyo maana hata katika ngazi ya kata, ofisi inaitwa ofisi ya ofisa mtendaji wa kata na si ofisi ya diwani.
Kwa maana hiyo, Dk Mahanga, ambaye kitaaluma ni mhasibu, alisema Rais alipounda Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ambazo awali zilikuwa mbili tofauti na kuteua makatibu wakuu watatu, kiuhalisia hakuunganisha wizara mbili kuwa moja bali ameunda wizara tatu kutoka mbili za awali.
“Ongezeko la gharama kwa kuongeza waziri mmoja ni ndogo sana kulinganisha na kuongeza katibu mkuu mmoja. Waziri anapoteuliwa tayari anakuwa ni mbunge mwenye mshahara wake wa ubunge na kinachoongezeka ni kama laki tano tu juu ya ule mshahara wa ubunge na gharama nyingine ndogo za gari, pia mishahara na gharama za katibu muhtasi, msaidizi na dereva,” alisema Dk Mahanga.
Alisema kwa ujumla ahadi ya Rais Magufuli aliyotoa kwenye kampeni kwamba ataunda Serikali ndogo, hakuitimiza badala yake ameongeza ukubwa wa Serikali.
Wakati wa kampeni na alipoapishwa, Rais Magufuli alisema ataunda baraza dogo la mawaziri, hiyo ilijenga shauku kwa wananchi kufahamu kiwango cha ukubwa au udogo wa baraza hilo ikilinganishwa na mabaraza yaliyoundwa na watangulizi wake, tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.
Dk Magufuli pia alitoa ahadi hiyo alipozindua Bunge Novemba mwaka jana mjini Dodoma.
7 comments:
Dr.Mahanga, umuache Mheshimiwa JPM afanye kazi yake. So far, so good and that is what the voters want. Wewe ni one of those losers and I can feel your pain.
Huyu Dr Makanga anyamaze tu. Akubali kukosa asianze kumwaga ujinga wake. Magufuli kupunguza mawaziri. Mwanche afanye kazi. Sisi watanzania tunataka matokeo. Mahanga alipewa fursa hatuna chochote cha kumkumbuka kufanya ama hata kujaribu kufanya. Tuliomaliza muda wetu tunyamaze tuwaaachie wengine.
ovyo.HUYU VIADO
Sasa jamani makatibu ndio mawaziri? Huyu jamaa katoka au kafukuzwa CCM kwa ubadhirifu na wakati CCM wanafanya kura ya maoni kutokana na mazaga zaga yake wakampiga na chini baada ya kuona hakubaliki CCM akakimbilia ukawa,kule ukawa kila jimbo alilojaribu kuomba kugombea ubunge kwa ticket ya ukawa akawaa anafukuzwa sasa leo eti kageuka mtaalamu wa kuunda serikali. Magufuli kwa kuteua makatibu wakuu wa kutosha kwa kila wizara amesevu gharama kwani katibu mkuu sio waziri.lakini vile vile amelenga kuzidisha ufanisi zaidi serikalini kwani makatibu wakuu ni field servants zaidi tofauti na mawaziri ambao mara nyingi tunaweza tukawaita house servants. Huyo makongoro mahanga he need to shut up, kwani alikuwepo kwenye serikali kwa miaka ishirini au sijui na zaidi mbona hatukumsikia akisema serikali ilikuwa kubwa,au bandarini na vyanzo vingine vya taifa vya mapato vinahujumiwa? Kwanini hatukumsikia akilalamika kuwa muhimbili kumeoza? Mwishoe yeye mwenyewe alipotaka kujihidhirishia kuwa ni mtu wa hovyo akaamua kuungana na lowasa. Wapizani walikuwa wako sawa kabisa kuhusiana na hali mbaya ya nchi wamekuja kuharibu na kutuuzi baada ya kumchukua lowasa aje kuongoza vita zidi ya mafisadi wakati yeye mwenyewe lowasa hapana shaka alikuwa kiongozi wa mafisadi ndani ya serikali ya CCM. Leo kwa mwezi serikali inakusanya 1 trillion na ushehe na makadirio ni kuongezeka zaidi kila siku zikisonga mbele alafu wanatokea watu ambao walishindwa kusimamia hata kile kijiofisi chake cha unaibu waziri ati sasa anakuja kujifanya yeye anaufahamu bora zaidi jinsi gani serikali inatakiwa iundwe? Ama kweli kama kusema ndio utendaji kwa watanzania basi hata Mungu angeliishangaa Tanzania kwa maendeleo. Tunawaomba wanasiasa uchwara wamuache muheshimiwa raisi afanye kazi yake kwa kweli yule magufuli yupo serious na anachkifanya na watu au watanzania bila ya kuweka usiasa mbele inatubidi lazima tu appreciate na kile anachokifanya kwani kinaonekana wazi hasa ukichukulia umri mchanga kabisa wa serikali yake kwani hata hajamalizia kuteua baadhi ya watendaji wake muhimu kama wakuu wa mikoa nakadhalika. Kukosolewa sawa lakini kwanza tutamtizama yule mkosoaji anasifa gani na vile vile kile kinachokosolewa kama kina kizi maslahi ya Taifa kama zitakosekana sifa hizo basi tutamuelewesha mkosoaji na watanzania kwa ujumla kwamba huo ni upuuzi mtupu.
BIG UP BULLDOZER, Mungu atakulinda baba.
Jamani hivi hamfahamu kwamba hata u-Dr wa Bw Mahanga ni wa kununua? Mtashangaaje ya mtu kama huyo?
Hata mtu asiye na cheti chochote anabusara kuliko huyu dr
Mahanga umefanya safi sana. Wala usiogope, you are very right. Matumizi yanakuja kuwa pale pale kama si kuongezeka zaidi
Post a Comment