Wednesday, January 13, 2016

FLAVIANA MATATA FOUNDATION YATOA MSAADA SHULE YA MSINGI MSINUNE

Taasisi ya Flaviana Matata ilizindua rasmi msimu wa "BACK TO SCHOOL" kwa kutoa vifaa vya shule kwa jumla ya watoto 270 wa Shule ya Msingi Msinune ambayo ipo chini ya ulezi wa mwanzilishi wa #FMF na mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata. Zaidi ya kutoa vifaa vya Shule Flaviana Matata Foundation kwa kushirikiana na wadau wamefanikiwa kujenga choo na waalimu na wanafunzi shuleni hapo. fmf msinune Flaviana Matata akikabidhi mabegi ya shule kwa watoto wa shule ya Msingi ya Msinune ambapo ameteuliwa kama mlezi wa shule hiyo kwa mwaka wa tatu sasa. fmf msinune primary school wanafunzi wa Shule ya Msinune wakikatiza na mabegi yao ambayo walikabidhiwa mwaka jana.    
FmF   fmf msinune 1
Flaviana Matata akikagua Choo cha wanafunzi kilichojengwa na FMF kwa msaada wa wadau. fmf msaada choo

No comments: