ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 28, 2016

Juma Duni Haji anauonaje utendaji wa Rais Magufuli?

5 comments:

Anonymous said...

Huyu mzee kweli jina lake halikukosea hata kidogo. Juma Duni? Kwa maana halisi ya kiswahili duni ni kitu dhaifu au pungufu. Kwa tunaemfahamu siku nyingi kule Zanzibar tunaelewa kiasi gani yu punguwani. Huyu ni mtu wa tamaa mbele na kuropokwa hovyo na ndio maana alinunuliwa na kifisadi na lowasa ili kwenda kujaribu kuwalaghi watanzania katika kinyang'anyiro cha kugombea uraisi. Huyu amepewa wizara ya afya kule Zanzibar ameiyangamiza kabisa na katika majipu basi huyu mzee sio jibu bali ni tenzi yaani hafai kabisa. Sasa leo uzalendo umemshinda baada ya kuona majibu wenzake yanatumbuliwa ati anasema yasitangazwe? Yaani mtu aibe alafu yule alieibiwa ndio aogope hata kusema kama ameibiwa, huyu mzee anaakili kweli? Aati ooh kuwatangaza hao walioibia serikali ni kuwafedhesha? Kwani walipokuwa wanaibia serikali hawakujua ni jambo la aibu? Hao wezi watangazwe ikiwezekana picha zao zibandikwe kila kwenye mikusanyiko ya umma ili iwe fundisho kwa wengine. Yaani huyu mzee ndie alikuwa anatarajiwa aje kuwa makamo wa raisi wa Tanzania kama lowasa angeshinda uchaguzi du! Jamani nchi yetu hivi sasa ingekuwa katika hali gani? Raisi fisadi msaidizi wake chizi. Nadhani hii ya mzee duni ya kuyaogopa na kuyaonea haya majizi kuyatangaza hadharani ni wasia muhimu aliopata kutoka kwa aliekuwa mgombea mwenza kwa tiketi ya uraisi muheshimiwa Lowasa kama tunavyojua lowasa alianza kuyapaka mafuta majipu mapema tu alipoanza kampeni zake za uchaguzi wa raisi. Kazi ya kuwakamata, kuwafukuza kazi,kuwafungulia mashtaka na kuwatangaza bila ya uwaoga wanahusika na vitendo viovu vya kuliangamiza taifa linahitaji kiongozi jasiri na ndio maana watanzania wamemchagua John pombe magufuli, lowasa na kama msaidizi wake wa uraisi angelikuwa huyu mzee hapo juu basi hata hivyo pele anavyosema magufuli anvitumbua, chini ya uongozi wao hata kuvikuna ingekuwa shida.

Anonymous said...

Yaani kwa maelezo ya huyu mzee anampa ushauri mueshimiwa raisi atulie ikulu tuli asiwe mfuatiliaji? Na vile vile anamtaka muheshimiwa raisi asiwe na haraka ya kufanya kazi yake kwa kuwa ana miaka mitano ya uraisi? Hivyo huyu mzee mawazo yake yalivyokuwa hafifu miaka mitano kaona muda mwingi sana wa kuzurura pale ikulu? Hii nchi imejaa uozo kila sehemu speed aliokuja nayo magufuli na viongozi wake mbali mbali aliowateuwa ni sahihi kabisa ili kuijenga Tanzania mpya. Tanzania ya watu wake kuwajibika ipasavyo,ile dhana ya kusema theres no hurry in Africa ndio iliotufikisha pabaya. Watu wazembe,wavivu,wezi, mtumishi wa umma anapigania kupata kazi serikalini dhamira yake kubwa ikiwa ni kwenda kuliibia taifa na kujineemesha yeye mwenyewe binafsi kuliko kwenda kulitumikia taifa na kupata malipo halali kutokana na kazi yake anaamua kutumia njia ya mkato ya kujitajirisha kwa njia za wizi hii hali imeota mizizi kwa watanzania na sasa lazima watu wabadilike la sivyo nguvu ya umma itumike kama tunavyoona katika uongozi wa mueshimiwa magufuli. Pamoja na ile dhana kulindana na kuoneana haya kwa viongozi wa umma waliohusika na kashfa za ufisadi kama huyu mzee anavyomsihi magufuli kwamba aache kuwatangaza hadharani hao mafisadi ni moja ya manbo yanayolea umasikini Tanzania na upuuzi wa hali ya juu.

Anonymous said...

Kweli wanasiasa wengi ni vigumu kuwaamini. Hivi huyu jamaa anaona tabu Magufuli kueleza kwanini anamfukuza Hosea ama Mkuu wa NIDA? Really? Mimi nilikuwa nawaona CUF watu wa maana; not any more!
Nini kimetokea kwenye uwazi na ukweli? Magufuli ni muwazi na mkweli. Tusimkatishe tamaa kwa ubinafsi wa wanasiaasa uchoro kama huyu Bwana. Wacha wasusie uchaguzi. Nilikuwa nawaonea huruma kumbe I was wrong! Mtu akifanya jema, kama Magufului, tukubali tu, sio kumlaani tena!

Anonymous said...

asanteni wote mmemaliza ,, lijinga kweli .

Anonymous said...

Magufuli oyee ila wafuadi wake asilimia 65 bomu!