ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 19, 2016

KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI YARINDIMA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA.

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mwanza leo imeahirisha Kesi ya Kupinga Matokeo ya Ubunge katika Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Novemba 25,2015 Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na Christopher Ryoba Kangoye ambae alikuwa Mgombea ubunge kupitia CCM katika Jimbo hilo.

Pichani ni Wakili Tundu Lisu (Katikati) ambae ni Wakili upande wa mjibu maombi wa kwanza ambae ni Mbunge wa Jimbo hilo John Heche akizungumza juu ya kesi hiyo baada ya kuahirishwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi January 27,2015 itakaposikilizwa tena.
Wakili Tundu Lisu (Katikati) ambae ni Wakili upande wa mjibu maombi ambae ni Mbunge wa Jimbo hilo John Heche akizungumza juu ya kesi hiyo baada ya kuahirishwa. Lisu aliiomba Mahakama kuifuta kesi hiyo kutokana na makosa mbalimbali ambayo ni pamoja na mleta maombi kushindwa kuainisha amefungua kesi kupitia sheria ipi ambayo inaitaka mahakama kufuta kesi ya uchaguzi.

Wakili Constatine Mutalemwa (Mwenye Miwani) anaetetea kesi hiyo kwa upande wa Mleta Maombi ambae anaiomba Mahakama hiyo kufuta matokeo ya Uchaguzi katika Jimbo la Tarime Vijijini kutokana na sababu mbalimbali ambazo ni pamoja kuhesabiwa kwa kura zisizo halali ambazo zilimpa ushindi Mhe.Heche. (Picha kutoka Maktaba)
John Heche ambae ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini kupitia Chadema (Wa pili kushoto) akiwa na wenzie nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza
Na:Binagi Media Group

No comments: