Askari wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Mwili huo kesho utaagwa nyumbani kwa Mwalimu Nyerere Msasani kabla ya kusafirishwa kwenda Butihama mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika keshokutwa.
Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani hapo.
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani hapo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
1 comment:
ukitaka mazishi ya kitaifa lazima uwe ccm
sina kinyongo na marehemu
lakini kama angekuwa cmm jeneza lingekuwa na bendera ya taifa
huyu hakuwa kiongozi wa kitaifa tusitumie bendera only kwa watu fulani
zanzibar wanasota leo RIP kisa karudi ccm na alikuwa mgonjwa miaka mingi
na mlimwabia ccm lazima arudi ccm ili mazishi yake yawe ya kitaifa
fuck cmm
Post a Comment