Tuesday, January 12, 2016

Leticia Nyerere kuzikwa Butiama.

Mbunge wa zamani wa viti maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Leticia Mageni Nyerere, aliyefariki dunia nchini Marekani, anatarajiwa kuzikwa kijijini Butiama, mkoa wa Mara.

Leticia ambaye ni mke wa mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Madaraka Nyerere, alifariki juzi katika Hospitali ya Doctors Community iliyopo Lanham, Maryland nchini humo na mwili wake utaletwa nchini na kuagwa jijini Dar es Salaam na kisha kusafirishwa kwenda kuzikwa Butiama.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na msemaji wa familia ya Hayati Mwalimu Nyerere, Makongoro Nyerere na kuongeza kuwa, mwili huo utaletwa nchini baada ya tataribu za kupata hati ya kifo kukamilika nchini Marekani.

"Mwili ukifikishwa jijini Dar es Salaam utakaa kwa siku moja ili wananchi watoe heshima za mwisho na kisha utasafirishwa kwenda nyumbani Butiama kwa ajili ya mazishi," alisema Makongoro na kuongeza:

"Tunaomba muendelee kutuvumilia wakati tukifuatilia ili kujua ratiba kamili ambayo itaonyesha ni lini mwili utarejeshwa nchini na hata siku yenyewe ya mazishi ambayo nimesema yatafanyika Butiama."

Alisema kwa sasa mdogo wake (Madaraka) na ndugu wengine wanaendelea na taratibu za kuurejesha mwili na kwamba serikali imeahidi kuusafirisha hadi nchini.

Kwa mujibu wa Makongoro, Leticia ni mtoto wa mzee Musobi Mageni na ameacha watoto watatu, mmoja wa kiume ambaye ndiye mkubwa na wawili wa kike.

Kabla ya kukumbwa na mauti, Leticia alikuwa ameiondoa Chadema na kurejea CCM Julai mwaka jana.

RAIS MAGUFULI AFARIJI FAMILIA
Rais John Magufuli jana amtembelea na kumpa pole mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere na familia yake kufuatia kifo cha mkwewe, Leticia.

Pamoja na kutoa mkono wa pole kwa Mama Maria nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli pia aliwapa pole wanafamilia wote na amewaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na ndugu yao.

CHANZO: NIPASHE

6 comments:

Anonymous said...

poleni sana wafiwa wote.kila nafsi itaonja mauti ametutanguliya na sisi tupo nyuma yake njiani.mungu ampe makazi mema huko mbele ya haki.amen.

Anonymous said...

Pumzika kwa amani dadangu Leticia!

Faustina said...

RIP dear Letty

Faustina said...

RIP dear Letty

Faustina said...

RIP dear Letty

Faustina said...

RIP dear Leticia