Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (pichani) kuanzia leo.
Aidha, baada ya utenguzi huo, Maimu amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao. Mkurugenzi wa Tehama, Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo, kuhusu uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
2 comments:
Huyo ndio Maghufuli kama msimamizi mkuu wa rasimali za watanzania tulimtarajia awe macho wakati wote kuangalia wapi kwenye jipu ili tumbuliwe haraka ili nchi ipate nafuu na kweli mueshimiwa raisi katuthibitishia kwamba kweli anaweza. Hongera magufuli.
Anaweza lkn kidole kimoja hakivunji chawa
Post a Comment