Thursday, January 21, 2016

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA CCM NEW YORK NA MAJIRANI


Chama cha mapinduzi- Tawi La NEW YORK na Miji ya jirani, tunapenda kutoa salamu za pole zilizojaa masikitiko makubwa kwa familia na ndugu wa Marehemu wa Mwenyekiti wa Tawi la CCM la DMV Mzee George Sebo. Pia tunapenda kutoa pole kwa uongozi wa chama wa tawi la CCM- DMV kwa kuondokewa na kiongozi wao mahili. Lakini pia tunapenda kutoa pole kwa watanzania wote wa DMV na wengine wote waliomjua marehemu na familia yake.
Tumesikitishwa na kuguswa sana na huu msiba hasa kwa kumjua marehemu kwa ukaribu sana, kwa mapenzi yake kwa watu wote na nchi yake. Kwa ukarimu wake kwa wanaccm na wasio wanaccm tunamjua marehemu kwa ukaribu yeye na mke wake na hata familia yake. Kama chama tutamkumbuka sana kwa kuwa mzee wa ushauri katika chama chetu na matawi yetu hapa Marekani. Tutayazingatia yale yote aliyotuachia na kuyafanyia kazi.

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un.

Seif Akida.

Mwenyekiti - Wa Tawi La CCM NEW YORK, NJ, CT, SPRINGFIELD,

1 comment:

Anonymous said...

poleni sana wana familia wote na wana ndugu wote na jamaa na watanzania wote including myself. poleni sana katika msiba huu. mungu amlaze mahali pema.amen

naomba kuliza kidogo mheshimiwa aliyefariki alikuwa muislamu au mkiristo?

hajalishi sote sisi ni watanzania ila kuna mtu katuma inna lillahi waina illahim rajiun ndo nataka tu kujua na si kwa nia mbaya.samahani kama nitakua nimekukwazeni kwa kuulza swali hili ila nauliza tu.

tupendane daima watanzania wote kwa dini na madhehebu yetu ndo hazina yetu hii.

poleni sana wafiwa wote vijimambo team thanks kwa kutuhabarisha habari hii