ANGALIA LIVE NEWS

Monday, January 11, 2016

UPDATES: MAALIM SEIF ASEMA KUWA HATAKUBALI UCHAGUZI KURUDIWA, UCHAGUZI KUFUTWA NI BATILI.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari juu ya Mustakabali wa hali ya kisiasa visiwani Zanzibar na hatua ambayo imefikiwa hadi hivi sasa.
Maalim anasema tume haina mamlaka ya kutengua matokeo bali ina mamlaka ya kurudia kuhesabu kura. Mwenyekiti wa tume Zanzibar alienda kinyume cha katiba kwa kufanya maamuzi bila kushirikiana na tume. Maalim anasema Katiba inasema "kila uamuzi wa tume ni lazima uungwe mkono na wajumbe walio wengi". Anasema katiba imetumia neno 'Lazima' na mwenyekiti kwenda kinyume inafaa kuchukuliwa hatua.
Pia Maalim Seif Sharif Hamad amemtaka rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli kuongoza mazungumzo ya kutatua mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani Zanzibar kwa kufuata misingi ya kikatiba na sheria baada ya mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea na Dr Ali Mohamed Shein wa CCM kwa kuwashirikisha marais wastaafu wa Zanzibar kutoonesha kuzaa matunda.

No comments: