Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene(Picha na Maktaba)
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George
Simbachawene amewasimamisha kazi wakurugenzi katika Mikoa ya Kigoma na
Katavi kwa ubadhirifu wa mali za umma.
Waliosimamishwa kazi ni
pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi
Bwn. Sulemani Lukanga kwa tuhuma za kununua gari hewa la kubebea
takataka kwa kiasi cha shilingi 92,750,000 na ubadhirifu wa fedha za
ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Kakese kiasi cha shilingi miambili
tisini na nne 294,000,000/=na .kinyume kabisa na sheria za utawala bora.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Eng. Boniface Nyambele anaetuhumiwa kwa
uuzaji wa nyumba za serikali bila kufuata sheria za uuzwaji wa mali za
umma.
Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameagiza nafasi ya Mkurugenzi wa
Manispaa ya Kigoma ikaimiwe na Mhandisi Sultan Imari Ndilowa ambaye ni
Mkuu wa Idara ya Maji, Manispaa ya Kigoma, nafasi ya Mkurugenzi wa
Manispaa ya Mpanda ikaimiwe na Ndugu Lauteri John Kanoni ambaye ni
Katibu Tawala Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Mheshimiwa
Waziri wa Nchi, amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Serikali
za Mitaa kote Nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao wafuate
Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Serikali haitasita kuchukua hatua
za kinidhamu kwa watumishi wote ambao watakiuka matakwa ya Sheria,
Kanuni na Taratibu na kutoweka mbele maslahi ya Umma.
Hatua ya
Waziri Simba chawene imefuatia ziara ya hivi karibuni ya waziri mkuu
Kassim Majaliwa ambaye alibaini matumizi mabaya ya madaraka na kuhitaji
ripoti kamili juu ya ubadhirifu uliofanywa na wakurugenzi hao.
No comments:
Post a Comment