ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 23, 2016

BARABARA YA KILWA; MFUPA ULIOMSHINDA FISI, KILA KUKICHA NI UKARABATI TU



BARABARA ya Kilwa, kipande cha Mtoni-Kwa Azizi Ali hadi Msikitini, kwa wale wenyeji wanajua maeneo hayo, imekuwa ni kama ile hadithi ya “Mfupa” uliomshinda Fisi.
Barabara hiyo imekuwa ikifanyiwa ukarabati karibu kila siku jambo la kusikitisha hata pale palipofanyiwa ukarabati napo panaharibika baada ya mudamfupi.
Ikumbukwe ya kwamba Waziri wa Ujenzi wakati huo, ambaye sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, alikataa kuipkea barabaar hiyo kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Tanguwakati huo, imekuwa ikifanyiwa marekebisho ya “kisanii” hapa na pale bila ya kukamilika. Pichani leo hii asubuhi Februari 23, 2016, Bwana huyu akielekeza magari katika eneo la ukarabati wa mtaro wa maji taka ambao huo tu peke yake umeshafanyiwa ukarabati zaidi ya mara tatu, chini kidogo ya daraja inakopita reli ya Tazara. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)


No comments: