ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 23, 2016

MFANYABIASHARA WA MCHELE ASHINDA SAFARI YA STARTIMES KWENDA UJERUMANI


 Mshindi wa droo ya pili wa promosheni ya Pasua  Anga na StarTimes, Bw. Johannes Maluli (kulia), akibonyeza kitufe cha kuchezesha droo ya kumpata mshindi wa tatu wa safari ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga. Wakishuhudia katikati ni Balozi wa kampuni hiyo kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda na Meneja Uhusiano wa Umma, Bw. Muddy Kimwery (kushoto).

Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akimwonyesha mshindi wa droo iliyopita (ya pili) ya kujishindia safari ya kwenda Ujerumani, Bw. Johannes Maluli (kulia) na waandishi wa habari (hawapo pichani) namna mshindi wa tatu wa promosheni ya Pasua Anga alivyopatikana. Akishuhudia droo hiyo kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Bw. Muddy Kimwery.

 Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mshindi wa tatu wa promosheni ya Pasua Anga ya kujishindia safari ya kwenda Ujerumani. Wakifuatilia kwa makini kulia ni mshindi wa droo iliyopita Bw. Johannes Maluli na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo, Bw. Muddy Kimwery  

Balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa vipindi na chaneli za michezo, Bw. Shaffih Dauda (kushoto) akimpongeza mshindi wa droo ya tatu, Johannes Maluli. 

Na Dotto Mwaibale

Bi Kisa Uswege (41) ambaye ni mfanyabiashara wa mchele mkoani Mbeya amebahatika kuibuka mshindi wa safari ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga katika promosheni iliyochezeshwa na kampuni ya StarTimes mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu Bi. Uswege alisema kuwa amefurahi sana kupata taarifa hiyo kutoka kwa kampuni ya StarTimes kwani hakutarajia kama angebahatika kujipatia fursa hiyo.

“Ninafuraha sana kupokea taarifa hii ya kuambiwa kuwa mimi ni mshindi wa droo ya bahati nasibu ya tatu ya wateja wanaotakiwa kwenda Ujerumani kushuhudia mechi ‘Live’. Nashukuru sana kwa ushindi huu kwa hakika nitaitumia hiyo fursa kwenda Ulaya kushuhudia mechi hiyo. Mimi ninaishi mkoani Mbeya na ninajishughulisha na shughuli za kuuza mchele, lakini fursa hii pia ninaimani itanifungulia mambo mengine.” Alielezea kwa furaha Bi. Uswege

“Mimi ni mteja mzuri wa StarTimes na huwa ninajiunga kila mwezi ili kupata chaneli na vipindi ninavyovipendelea. Kila mwezi lazima nilipie ili nifurahie vipindi vyangu au wakati mwingine kwa ajili ya watoto wangu,” alisema na kumalizia Bi. Uswege kuwa, “Kwa mfano huwa naangalia chaneli za mipira, filamu za kihindi na kinaijeria. Watoto wangu wao wanapendelea sana chaneli na vipindi vya Kung Fu, StarTimes Swahili Bollywood na Novela E1. Kwa mfano hapa nyumbani huwa tunapenda sana chaneli ya Star Swahili Bollywood kwani filamu zake zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na kutufanya tuelewe”

Naye kwa upande wake Meneja Uhusiano wa kampuni ya StarTimes Tanzania aliongezea kwa kusema kuwa promosheni hiyo ni ya kweli na haina upendeleo wa aina yoyote ndiyo maana washindi wanatoka maeneo mbalimbali zilipo huduma za kampuni hiyo.

“Wiki iliyopita tulishuhudia mshindi wa droo ya pili akitokea mkoani hapa Dar es Salaam lakini safari hii ni mama kutoka Mbeya. Promosheni hii inafanyika kwa kuhusisha wateja wetu wote nchini ukizingatia atumesambaza huduma zetu takribani mikoa 18 sasa. Ningependa kuwasihi wateja wetu wazidi kulipia vifurushi vya mwezi kwa kuanzia na kiasi cha shilingi 5000/- tu na kuendelea na wengine wajiunge nasi kwani kwa kufanya hivyo watakuwa waeunganishwa na droo hii moja kwa moja.” Alisema Bw. Kimwery

Kwa kumalizia Meneja Uhusiano huyo wa StarTimes alisema, “Nawataka wateja na watanzania kufuatilia droo hiyo ya bahati nasibu kila mwishoni mwa wiki kwani yeyote anaweza kuwa mshindi. Na pia nawaomba simu zenu ziwe hewani au kupokea pindi mpigiwapo kwani mnaweza kupoteza bahati.”

No comments: