Watu 7 wamefariki na wengine zaidi ya 56 wamejeruhiwa katika ajali basi mkoani Mara.
Watu saba wamafariki wamefariki dunia na wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la nata raha yenye namba za usajili T 473 CJN linalofanya safari zake kati ya Mugumu wilayani serengeti kupitia Bunda kwenda mkoani Mara kupalamia nyumba eneo la njia nne mjini Bunda baada ya breki za basi hilo kukatika likiwa katika mteremko mkali.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamedai baada ya kukaribia njia kuu ya Mwanza Musoma mita chache tu kufika kituo kikuu cha mabasi mjiniBunda mwendo wa basi hilo uliongezeka na baada ya kuhoji walielezwa kuhusu kukatika kwa breki hizo kabla ya kuvamia jengo hilo.
Hata hivyo wakati mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama akisema walifariki ni abiria saba lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mara ACP Philip Alex Kalangi akizungumza na ITV kwa njia ya simu amesema abiria sita ndiyo waliofariki katika ajali hiyo.
CHANZO: ITV TANZANIA
No comments:
Post a Comment