Tawi la Chama Cha Mapinduzi nchini
Uingereza, wamepongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa uthubutu na kasi
ya hali ya juu ya kurekebisha mfumo wa utendaji katika serikali ambapo umekuwa
na uozo mwingi na wa muda mrefu uliopelekea wananchi hasa wa hali ya chini
kukosa huduma za muhimu kutokana na watendaji wengi kufanya kazi kwa mazoea
yaliyopelekea kuzorota kiufanisi.
WanaCCM hao wa Uingereza wamesema kuwa
siku zote serikali ya CCM imekuwa ikipata lawama nyingi katika utendaji mbovu
na hivyo kupelekea wananchi kukata tamaa na utendaji wa Serikali na Chama
chenyewe ili hali ni baadhi tu ya watendaji wachache wabovu waliokuwa kwa
makusudi mazima wanatenda kazi zao chini kiwango bila weledi ama kwa makusudi
ili tu kuharibu sifa ya Chama Cha Mapinduzi.
1 comment:
Labour Party UK tawi la Kigogo lampongza Prime Minister wa UK.
Post a Comment