ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 2, 2016

DC KINONDONI, PAUL MAKONDA APOKEA SARUJI MIFUKO 1640 KUTOKA KWA WADAU WA MAENDELEO KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARY

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Duma, Areeq Amran Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mfuko mmoja wa saruji kati ya 640 aliyoitoa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari za wilaya hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Katika makabidhiano hayo Makonda alipokea mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Alex Malasusa aliyetoa mifuko 500. 
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo (kulia), akimkabidhi saruji hiyo DC Makonda.
Lori lilibeba saruji hiyo likiwa eneo la tukio.
DC Makonda na wageni wake wakiwa eneo la tukio kabla ya makabidhiano ya saruji hiyo.
Mhe. Bulembo akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo.
Wanahabari wakizungumza na watoa msaada huo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)


Na Dotto Mwaibale

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi, Abdallah Bulembo amesema anaguswa na kazi nzuri ya utekelezaji wa Ilani ya CCM inayofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda katika ujenzi wa shule za sekondari za kata.

Bulembo ambaye pia ni Mjumbe wa kamati kuu ya CCM alisema kutokana na jitihada hizo ameona haja ya kumtia moyo Makonda kwa kuchangia ujenzi wa shule hizo saba unaoendelea.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kukabidhi saruji mifuko 500 Bulembo alimtaka Makonda kuendelea kupigania utekelezaji wa Ilani bila kujali itikadi za vyama katika kuleta maendeleo ya wilaya hiyo.

Alisema Jumuiya ya wazazi kazi yake kubwa ni ulezi hivyo mafanikio yatakayopatikana kutokana na wanafunzi zaidi ya 3183 waliokosa shule katika wilaya hiyo kuweza kuendelea na masomo ni ya kujivunia.

Aliwataka watendaji wa Manispaa hiyo kuhakikisha malengo ya ujenzi huo yanatimia ili kuokoa watoto ambao wangeathirika kutokana na kukosa elimu.

Makonda aliwapongeza wote wanaojitokeza katika kumuunga mkono katika ujenzi wa shule hizo na kusema jana amepokea mifuko 1640 ya saruji.

Alisema saruji hiyo ni mifuko 500 kutoka kwa Bulembo,500 kutoka kwa aliyekuwa Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Alex Malasusa na mifuko 640 kutoka Kampuni ya The Duma Group.

Aliwahakikishia wadau hao wa elimu kuwa atasimamia ipasavyo ujenzi wa shule hizo ili kupunguza wimbi la watoto wasio na elimu Kinondoni ambao ndio chimbuko la vijana wanaotumia dawa za kulevya,biashara ya ngono,vibaka,mimba za utotoni na wahalifu wengine.

Mkurugenzi wa Kampuni ya The Duma Group, Areeq Amran Mohamed alisema lengo la kusaidia saruji hiyo ni kuungana na serikali katika kutekeleza sera ya kuinua elimu wilaya ya Kinondoni.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

1 comment:

Anonymous said...

Hips unazo Makonda