Msomaji wa Gazeti la Uwazi wa eneo la Temeke Mwembe Yanga, Japhary Maleku (katikati) akijaza kuponi yake. Anayeshuhudia kushoto ni Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda na msomaji mwingine pembeni yao akiwatazama.
Msomaji wa Gazeti la Uwazi, Shaban Jumanne (kushoto) akijaza kuponi yake ili kushiriki droo ya pili inayotarajiwa kuchezeshwa Alhamis.
Shaban akivalishwa kofia yenye nembo iliyoandikwa Shinda Nyumba kutoka kwa Ofisa Masoko,Yohana Mkanda.
Doto Ally (kushoto) akivalishwa kofia iliyoandikwa' Shinda Nyumba' kutoka kwa Yohana Mkanda baada ya kujaza kuponi yake ili kushiriki droo ya pili.
Wasomaji wa eneo la Temeke Mwembe Yanga wakichangamkia kununua magazeti ya Uwazi kutoka kwa muuzaji wa kampuni ya Global (mwenye fulana nyeupe) ili kushiriki droo ya pili itakayochezeshwa kesho.
Mwajuma Kasim (kulia) akijaza kuponi yake ili kushiriki droo hiyo itakayochezeshwa kesho. Anayeshuhudia katikati ni Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkana.
Msomaji wa Gazeti la Uwazi wa eneo la Tandika sokoni, Mwamini Aly (kushoto) akivalishwa kofia yenye nembo iliyoandikwa Shinda Nyumba na Ofisa Masoko wa Global.
Wasomaji wa eneo la Tandika Sokoni walivyoonekana kuchangamkia magazeti ya Uwazi kwa kujaza kuponi ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba itakayochezeshwa kesho.
Mdau wa Gazeti la Uwazi aliyejitambulisha kwa jina la Athuman (kulia) akielekezwa na Ofisa masoko wa Global,Yohana Mkanda (kushoto) namna ya kujaza kuponi yake ili kushiriki droo hiyo.
Wasomaji wakishiriki kuweka kuponi zao eneo la Temeke.
Wasomaji wa Gazeti la Uwazi wakiendelea kujaza kuponi ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba eneo la Temeke Mwembe Yanga.
Muuzaji wa Magazeti ya Global, (kushoto) akimwelekeza msomaji namna ya kujaza kuponi ili kushiriki droo hiyo.
Msomaji wa Gazeti la Uwazi, Mbushi Elisha (kulia) akijaza kuponi kwa ajili ya kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba.
Mpenzi msomaji wa Uwazi aliyejitambulisha kwa jina la, Haidary Rashid (kushoto) akijaza kuponi baada ya kununua
Mwanadada aliyehamasika na bahati nasibu hiyo, Zainab Omary akiweka kuponi.
LILE Shindano la Shinda Nyumba linaloendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani, Ijumaa Wikienda na Championi linazidi kushika kasi ambapo kesho Alhamisi, Februari 18, mwaka huu droo ya pili itafanyika Mchikichini, Karume, Ilala jijini Dar.
Akizungumza na gazeti hili Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda aliwataka Watanzania kuendelea kununua magazeti hayo kwa wingi na kukata kuponi ili waweze kujiongezea nafasi ya kushinda.
“Wewe msomaji unatakiwa kununua gazeti lolote linalochapishwa na Kampuni ya Global Publishers kisha unajaza kuponi itakayokuwezesha kushiriki droo hiyo ya pili ambayo utajishindia zawadi mbalimbali,” alisema Mkanda.
Katika droo hiyo zawadi zitakazotolewa ni pamoja na runinga zenye kioo bapa, ving’amuzi vya TING, vyombo vya jikoni, mashuka na zawadi nyingine kibao, watoto walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki shindano hili.
NA DENIS MTIMA/GPL
No comments:
Post a Comment