Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva amewataka wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu waache kujitangaza kuwa walishinda, akisema wanapotosha wananchi.
Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kudai kuwa kama si matokeo kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.
Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari ofisini kwake, akisema yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.
Jana, akiwa kwenye mkutano wa tathmini kati ya NEC na asasi za kiraia kuhusu utoaji elimu kwa mpigakura uliofanyika Dodoma, Jaji Lubuva alisema uchaguzi umeshapita na kilichobaki sasa ni kufanya kazi tu.
Bila ya kutaja jina la mwanasiasa huyo, Jaji Lubuva alisema kama kuna mtu alishindwa katika uchaguzi uliopita, ajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.
“Hata wananchi wanawashangaa kwa kuwa wao ndio walioamua ni nani anafaa kuwaongoza,” alisema Jaji Lubuva.
Alisema kuwa NEC ilikuwa inapokea matokeo ya uchaguzi kutoka majimboni na kuyasoma kama yalivyotumwa na katika hilo hakuna wakala hata mmoja wa chama ambaye aliyapinga matokeo hayo.
“Sasa nashangaa kuna baadhi ya wagombea wanaotaka Tume ifukuzwe kazi eti tu kwa sababu wao hawakushinda. Naomba ifahamike kwamba katika kila uchaguzi duniani kuna kushinda na kushindwa.
"Sasa kama kila atakayeshindwa atataka tume ifukuzwe kazi hapatakuwa na tume ya uchaguzi kwa sababu kila atakayekuwa anashindwa atakuwa anataka tume ifukuzwe kazi,” alisema Jaji Lubuva.
Chadema, ambayo iliungana na vyama vitatu kuunda Ukawa, iliitaka NEC kusitisha utangazaji matokeo ikidai kuwa kilichokuwa kikitangazwa ni tofauti na takwimu walizokusanya kutoka majimboni. Lakini NEC ikaendelea kutangaza.
Baadaye, Chadema ililalamika ikidai kituo chao cha kukusanya na kujumlisha matokeo kilivamiwa na polisi na kompyuta kuchukuliwa na hivyo kuvuruga ufuatiliaji wao wa matokeo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa huduma kutoka NEC, Emmanuel Kavishe alisema kuwa Tume inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na Katiba na kwamba hata siku moja haijawahi kumpendelea au kumuonea mtu yeyote.
Katika uchaguzi wa urais, John Magufuli alipata kura milioni 8.8 huku Lowassa akipata milioni 6.07.
9 comments:
Asante jaji wa tume ya uchaguzi ya Chama tawala! Hakuna kisichoeleweka katika uchaguzi uliopita na njama ambazo zilipangwa na tume kwani hali halisi ilikuwa kuwanyamazisha wasimamizi na wataka haki nchi nzima kudai matokeo. Haya yaliandaliwa bila ubishi kwani namba zilikinzana sana ila hakukuwepo haki kuuliza walamkudai. Wewe ulikuwa unasoma.namba zilizoandaliwa sasa hayo matokeo.uliyokuwa mnapokea ilikuwa kiasi cha kubadili namba! Anyway hakuna jinsi chama au kikundi kinaweza kulisemea kwani si matarajio si yalishakamilika! Tusonge mbele kwani yaliyotendeka Zanzibar ni mfano na sasa hivi uchaguzinwa marudio namba zilishapangwa tayari. Kinachofanyika ni kiini macho tu na kuonyesha dunia kuwa tumeshinda! Ila kwa wizi wa kura. Kazi tuh!!
Hata siku moja watanzania hawawezi kuacha kumchagua mtu muadilifu na mchapa kazi kama maghufuli waende wakamchague mgonjwa wa afya,mtuhumiwa wa ufisadi uliokisiri,mtu ambae alikuwa yupo tayari hata kuwabagua watanzania kwa misingi ya udini na ujimbo ili yeye awe raisi watanzania wengi akili zao hazijaoza kiasi hicho kushindwa kufahamu kizuri na kibaya mchana kweupe. Muacheni huyo aliejiapiza lazima awe raisi katika maisha yake aendelee kuweweseka kwani ameshagundua yakuwa kuna mazezeta fulani ya kitanzania hata akiyaambia kuwa yeye ni Yesu basi wataamini licha ya kiongozi huyo kuwa na dalili zote za ushetani. Watanzania bila shaka walishaichoka CCM na ukitaka kujua kwanini watanzania waliichoka CCM angalia mambo yakifisadi yanayoibuliwa na serikali ya maghufuli utajua yakwamba watanzania sio wajinga bali kwa heshima ya CCM miongoni mwa watanzania ilibidi wakipe muda wa kujisahihisha lakini kila siku zilivyokuwazukienda mbele viongozi wao walishindwa kujitambua na kweli watanzania walishafikia mahala kufanya maamuzi magumu kumtafuta mbadala wa CCM kuingoza nchi ila tatizo wapizani nao walishindwa kuwaelewa watanzania wanataka nini. Katika hali ya kawaida huwezi kuwaletea wagonjwa mtu wanaemtuhumu ndie aliewaroga kuwa ndie mtu sahihi kuwaondoshea matatizo yao huko ni kucheza na akili za watu.siku ukawa unampa lowasa nafasi ya kugombea uraisi ndio siku watanzania wa ndani na wanje walipokata tamaa yakuwa wapinzani kama kweli wapo serious kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania?
Kwani kama kikwete kama lowasa next online angaendelea kuendesha nchi kwa njia ya mazoea haijalisi chama gani yupo.Watanzania walikuwa wanamtafuta kiongozi mwana mabadiliko wa kweli na haijalisi anatoka chama gani. Kiongozi ambae ikiwezekana kutokea CCM lakini nje ya CCM inner circle Kiongozi ambae asiekuwa na kigugumizi kulaani na kupiga vita rushwa wizi wa mali ya uma,ubabaishaji seriakalini na kuwaondoshea umasikini wananchi katika nchi tajiri iliojaa rasilimali. Fikiria hili jambo moja la kiuchumi ambalo nchi yetu kwanini iwe maskini? Uganda,DRC,MALAWI,RWANDA,BURUNDI,ZAMBIA,nchi zote hizo zinauwezo wakutumia bandari za Tanzania kikamilifu kama kutakuwa hakuna ubabaishaji wa huduma na mizigo yao kuibiwa. Kama ningekuwa magufuli basi kila katika hizo nchi zinazotumia bandari zetu ningewatengea bandari yao ndani ya bandari ya Tanzania na watu wao na bendera yao katika eneo lao husika sisi kazi yetu kuhakikisha kodi yetu tunaipata kikamilifu,ndio mteja wa biashara ni mfalme mtunze waswahili wameliona zamani sana hilo. Na kuhusu Lowasa na Magufuli? muangalie magufuli hata hao wana CCM wenzake wabazirifu matumbo joto ni kiongozi dream ya watanzania kwa muda mrefu sasa yeye huyo Lowasa hata anachokiongea hakieleweki zaidi ya ubinafsi uliomjaa wa kuendekeza umimi kwani anachokifanya magufuli lowasa hata robo yake asingeweza kufikia.
Jaji Lubuva, unatumiwa na CCM na hujasema ukweli kabisa katika uliyoongea hapa. Ni wazi katika maongezi yako hata hukumu ulizowahi kutoa huko nyuma zina walakini. Lakini yote tisa, hapa duniani tuna pita tu, ccm haipo kutangaza hat miliki ya nchi hii. Tubadilishe katiba tuone mtakuwa wapi nyie vibaraka wa ccm na ccm yenyewe. Mnataka hata kuwanyima kafu ushindi wao sisi wananchi tunaoona. Mnapeleka jwtz hatuoni? Unasikiliza htouba ya magufuli wakati wa Feb5, je husomi hayo maneno ya raisi magufuli?
Si ndio huyuhuyu Lowasa aliwaambia watu waliokuwa wanamtuhumu kwa ufisadi watoe ushahidi au wanyamaze.Nadhani,likewise Lowasa anapaswa kuumwaga ushahidi hadharani na kama hana he needs to shut up once & 4 all.
Watanzania wengi tulio na usongo wa maendeleo ya nchi yetu na ambao kwa muda mrefu tulikuwa tunasubiri ujio wa kiongozi mwenye mwelekeo kama wetu sasa tumempata na kazi ya kutuletea maendeleo hayo ameshaianza. Pamoja na haya yote, kiongozi huyu hivi karibuni tu ametutangazia pia kuwa ule mpango wa uanzishaji wa mahakama maalamu ya kushughulikia mafisadi na wahujumu uchumi kama alivyotuahidi, karibu itamalizika na hivyo wahusika wa vitendo hivyo viovu waanze kujiandaa. Sasa wale ambao hawaamini kuwa Mheshimiwa Magufuli aliyechaguliwa na Watanzania wengi na wala hakupewa madaraka haya na Jaji Lubuva kama sadaka, wacha waendelee na ubishi wao. Ila ni lazima wajue tu kuwa idadi kubwa ya Watanzania hadi leo iko vijijini na ndiko ambako kura nyingi rais alikozipata. Wazo la kuwa na ushindi wa kura katika miji miwili au mitatu tu hata ikiwa miji yenyewe ni mikubwa namna gani, idadi ya kura zinazopatikana kwa kila mgombea haziwezi kutosheleza kumpatia kura kiongozi yeyote yule na kumfanya ashinde kama hatakuwa ameshirikisha idadi ya watu wengi waishio vijijini. Hili ndilo kosa ambalo akina Tomaso hawataki kulielewa na hivyo wanaendelea kung'ang'ana kuwa walishinda na kuitaka dunia iwaelewe kuwa wameonewa. Na kama hawatataka kujisahihisha na kutafuta ufumbuzi wa swala hili wataendelea kulalamika muda wao wote hata kama katiba itabadilishwa kama wanavyotaka. Wasifikirie kuwa kupeleka kesi mahakama ndiyo mahakama itampa mtu ushindi kwa ajili yeye ni mlalamikaji tu. Lazima kuwe na hoja na ushahidi unaoambatana na malalamiko. Na kwa ajili sasa "hapa ni kazi tu" lile swala la mlungula haliko tena hivyo mahakimu nao watataka kutenda kazi zao kwa haki kama somo lao linavyowaelekeza.
Huyu Lubuva ni puppet kabisa wa CCM na ni aibu kabisa kwa Taifa kuwa na majaji wa namna hii.Yaani badala ya kusimamia haki za wananchi anatumia fani na nafasi yake kukandamiza haki za wananchi.Ni lazima jaji atambue kuwa wananchi wa sasa wameamka siyo wale wazamani.
Kwa mfano,Mwaka 2005 CCM ilishinda kihalali kabisa na JK alipata asilimia 81 ya kura zilizopigwa na hata wapinzani wanajua hilo. LAKINI UCHAGUZI WA MWAKA 2015 CCM HAWAKUSHINDA KWENYE URAISI NA HUO UTABAKI KUWA UKWELI HATA KAMA LUBUVA NA CCM WATAENDELEA KUTISHA WAPINZANI na kusema ukweli tunawapongeza wananchi kwa kuwa na busara na kuamua kulinda amani ya nchi LAKINI UKWELI UNABAKI KUWA UKWELI.
Upinzani mliahidi kupeleka kesi Mahakama ya Kimataifa kama hamtatendewa haki. Uchaguzi umeisha na rais kapatikana. Bahati mbaya hamkushinda ila mmebaki kulalamika kuwa mmeonewa mkidanganya umma wa Watanzania na dunia nzima kuwa mlishinda. Kama kweli mlishinda mbona hamtupi idadi kamili ya kura zenue zinazoonyesha ushindi na ambazo zitakuwa zinatofautiana na idadi zilizotolewa na Tume chini ya Jaji Lubuva! Na kama kweli tatizo ni sheria za nchi kuwabana, kwa nini sasa hampeleki hoja yenu kwenye Mahakama ya Kimataifa ambayo mlikuwa mnaiongelea kila mara wakati wa kampeni zenu! Au mmeshaanza kuhisi pia kuwa kwenye mahakama hiyo nako kuna mkono (au ni puppet) wa CCM?
Jamani siasa za Tanzania bado za maji taka ona huko Zanzibar!.. Sisi Tunaangalia tu. Ngoja tuone mwisho wake! Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Siasa za Tanzania siyo bado za maji. Tatizo ni pale panapokuwa na viongozi ambao wanafikiria kuwa kukusanya watu wengi kwenye mikutano ndiyo dalili za ushindi bila kuelewa kuwa watu wanakwenda kwenye mkutano kumtathimini mgombea ili baadae iwasaidie kufanya maamuzi ya nani kumpa kura zao. Pia kuna wengine wanakwenda kwenye mkutano tu ku-pass time au kujumuika na rafiki au jamaa zao na pia kuna wengine ambao umri wao hauwaruhusu kupiga kura. Pamoja na hayo kuna wengine baada ya mikutano ya kampeni kufanya wankuwa wamekata tamaa na hivyo hawaendi kupiga kura. Kwa hiyo idadi kubwa ya wanaohudhuria mikutano ya kampeni siyo ya kugezo kikubwa cha kujitangazia ushindi. Ni muhimu kungojea idadi kamili inayotolewa na vyombo vinavyohusika. Kama kuna tatizo kuwe na uwazi wa kulinganisha idadi ya kura zitolewazo na vyombo husika na zile ambazo vyama vya kisiasa vinakuwa vimejijengea. Kulalamika tu kuwa washindi kwa kura kadhaa au asili mia kadhaa bila kutoa ufafanuzi unaoambatana na tarakimu zinazoonyesha jinsi kura zilivyopatikana haisaidii. Hakika tutafika na Mungu Ibariki Tanzania na tubariki Watanzania wote kwa ujumla wetu.
KWA BLOG AUTHOR: Kwa nini unaweka nembo ya "delete comment" kwenye makala zangu wakati makala za wengine huweki?
Post a Comment