ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 22, 2016

MAKONDA, MEYA CHADEMA WAVUTANA KWA UTENDAJI

Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob na Mkuu wa wilaya hiyo, Paul Makonda wameingia kwenye mvutano kuhusu kuvuka mipaka ya utendaji wa halmashauri hiyo.
Mvutano huo umekuja baada ya Jacob kumtuhumu Makonda kuwa ametoa taarifa za kikao cha kamati za fedha ya halmashauri hiyo kilichofanyika wiki iliyopita kinyume na taratibu.
“…Tena hata kwenye kikao hakuwepo, lakini nashangaa kuona ameenda kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa Wilaya ya Kinondoni inatarajia kupata dola 300 milioni za Marekani sawa na Sh600 bilioni kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya miradi ya maendeleo,” alisema Jacob jana kwenye mkutano na waandishi wa habari.
“Vikao vyote vya halmashauri ni siri…huo ni upotoshaji na Makonda anaingilia mamlaka zisizokuwa za kwake, ” alisema.
Jacob alisema halmashauri hiyo imeshindwa kufumbia macho jambo hilo kwani linaweza kuleta mvutano baadaye.
“Mimi nalalamikiwa na wajumbe wa kamati, wanasema kwa nini taarifa za kikao ambazo ni za siri zinatangazwa wakati bado michakato yake inaendelea?” alihoji Jacob.
Meya huyo alisema Makonda ambaye alipewa taarifa hizo na maofisa tarafa waliohudhuria kikao hicho, alitakiwa kuuliza uongozi wa halmashauri kabla ya kutangaza kwa umma.
“Sasa leo ikitokea wajumbe wamegoma kupitisha maazimio kuhusu mchakato huo hizo hela atatoa wapi?” aliendelea kuhoji.
Alisema endapo Makonda ataendelea na tabia hiyo, maofisa tarafa watazuiliwa kuhudhuria kwenye vikao vya kamati za fedha za halmashauri hiyo.
Hata hivyo, Jacob alisema si mara ya kwanza kwa mkuu huyo wa wilaya kuvuka mipaka na kuingilia shughuli za halmashauri, ambazo kimsingi zinapaswa kufanywa na meya, mkurugenzi au msemaji wa halmashauri.
Meya huyo alisema mara ya kwanza Makonda alisema halmashauri itajenga machinjio ya kisasa, wakati anafahamu hana uwezo wa kupata fedha za kufanikisha mradi huo.
Jacob alisema halmashauri ndiyo yenye dhamana na kuidhinisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.
Pili, aliwahi kuwaita wenyeviti wa Kinondoni Leaders Club kwa ajili ya kuzungumzia mchakato wa kuvunja maeneo ya wazi yaliyojengwa.
Gazeti lilipomtafuta Makonda kueleza kuhusu madai hayo, alisema Jacob bado ni mwanafunzi hivyo hawezi kuzungumza chochote juu ya madai hayo.
“Amechaguliwa kuwa meya juzi tu bado mwanafunzi, hafahamu mipaka ya mamlaka yangu. Akijifunza na kuelewa hizo kelele hamtazisikia tena,” alisema Makonda.

MWANANCHI

4 comments:

Anonymous said...

Hivi kuna usiri gani katika kupokea fedha za maendeleo kutoka Benki ya Dunia? Watu wasiozoea uwazi wana matatizo ya uongozi. Bwn Makonda hajafanya ouvu wowote ule kutoa taarifa ya matarajio ya mapato ya wilaya. Shida ni kwa wale waliokaa mkao wa kula. Mambo yamebadilika. Hongera Magufuli.

Anonymous said...

Haya ni malumbano yasiyo na tija. Benki ya dunia inaikopesha au kuisaidia Serikali, ambayo ikipata ahadi hio huwasiliana na mikoa na wilaya husika. Mkuu wa wilaya atakuwa kapewa taarifa za kiserikali maana sio siri. Na Msaada au mkopo huo una masharti na maelekezo ambayo vikao vya mikoa au wilaya inapofanyika miradi hio bila makubaliano ya mfadhili.
Fanyeni kazi pamoja sio showdown hapo!!!

Anonymous said...

Heee!!! Huyu Meya anasahau hapa kazi tu. Hmna siri katika mambo ya hela kwanza ni huku kwetu tu Africa hizo siri nchi zilizoendelea wanatangaza magazetini na zitatumikaje eeeeh!!! Atasubiri sana huyo meya kile cha kupiga panga la uvunguni kimekwisha. Kwani mueshimiwa wa sasa Tanzania ni mchapa kazi na anaejielewa yule wa kulanda landa na kula starehe alikuwa hataki umiza kichwa hakuwa kikazi zaidi muda wake ulishakwisha na ndio maana mambo yote yalikuwa yanaenda vise vesa. Weee Meya hapa kazi tu. Cha kupiga panga kimepitwa na wakati. Mwenzako yuko sawa kabisa kikazi

Anonymous said...

Meya wa chadema huyoo.... Eti siri nyoko hakuna siri hapa ni kazi tu. Hizo ni public record siri ya nini we kilaza meya. Na mkuu wa wilaya ana mamlaka kamili ya kuipngelea wilaya yake. Na meya na madiwani mnaripoti kwake, kweli bado mwanafunzi. Ulifikiri hii awamu ya kula, hapa kazi tu na hakuna siri ndio maana tunatbua majipu hadharani wananchi wajue. Mambo kama dunia ya kwanza uwazi tu. Siri fanyeni ndani ya chama chenu au nyumbani kwako.