Masanja Mkandamizaji amezindua Mgahawa wake wa Kisasa kwa kuandaa sherehe za uzinduzi kwa kuwakaribisha wadau mbalimbali Mgahawa huo unaoitwa “Masanja Wali Nyama” upo maeneo ya Tabata Magengeni Karibu na Benki ya CRDB BANK.
Shughuli hiyo iliyo anza saa mbili usiku na kumalizika saa tano usiku, ilipambwa na waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili akiwemo Miriam Jackson, Emmanuel Mbasha, Faraja Ntaboba, Mc Makondeko, Stella Joel pamoja na Wachungaji, Mitume na Manabii.
Huku pia wakiwepo wasanii waigizaji mbalimbali ambao walifika kwa ajili ya kumsapoti msanii huyo majasirimali ambaye licha ya kumiliki mgahawa huo Masanja pia ni mkulima mzuri mwenye mashamba ya kulima Mpunga makubwa tu, hivyo amezidi kupaa zaidi Hongera sana.
No comments:
Post a Comment