ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 16, 2016

Tundu Lissu Matatani Ahojiwa na Polisi Lisaa Limoja Kisa Gazeti la Mawio lililofungiwa


TUNDU Lissu, Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pia Mbunge wa Singida Magharibi leo jijini Dar es Salaam amehojiwa na Jeshi la Polisi kuhusu hoja alizozitoa kwenye Gazeti la MAWIO, anaandika Faki Sosi.
Lissu amehojiwa kwa zaidi ya saa moja Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kuhitajika kutoa maelezo kwa madai ya kutoa kauli za uchoelezwa zilizoandikwa kwenye Gazeti la MAWIO zilizohusu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Habari iliyoandikwa na gazeti hilo iliyobeba kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’ inaelezwa kuwa sababu ya serikali kulifungia gazeti hilo tarehe 15 Januari mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutoa maelezo Lissu amesema, serikali inajaribu kumziba mdomo asizungumzie kuhusu suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani Zanzibar wakati wahusika hawazingatii misingi ya demokrasia.

“Wale waliobebwa kwenye uchaguzi leo wanataka kutufumba midomo tusizungumzie masula ya uchaguzi wa Zanzibar kwani machafuko yanaweza kutokea visiwani humo kwa tahadhari hiyo wanatuita wachochezi,” amesema Lissu.

Amesema kuwa, wao wametoa tahadhari ili yasitokee machafuko na umwagikaji wa damu na kwamba, Rais John Magufuli atawajibika kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kama alivyowajibishwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Amesema, mahojiano yake na Gazeti la Mawio ndio yaliyosababisha yeye kuitwa na kuhojiwa na polisi na kwamba, mtazamo wake ulioandikwa kwenye gazeti hilo ndio umechangia kufutwa kwa gazeti hilo.

Amesema kuwa hatokubali kuzibwa mdomo hata kama watatumia nguvu ya polisi.
Amesema, hatua ya Rais Magufuli kukakataa kujihusisha na mgogoro wa Zanzibar haikubaliki kwa kuwa ndiye ndiye atakayepeleka jeshi pale vurugu zitakapotokea.

Lissu amefika polisi hapo akiwa na mawakili wa watatu wa Chadema ambao ni Peter Kibatala, Fedrick Kiwelo na Hekima Mwasibu.

Amesema, baada ya mahojiano hayo polisi watapeleka jalada lake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa hatua zaidi.

5 comments:

Anonymous said...

Huyu Lissu ni kibaraka (puppet) wa wazungu na waarabu ambao hawalitakii mema Taifa letu. Yaelekea wamekwishamuhaidi mabilioni as long asili anafungua domo lake kama kasuku, na ninaamimi wanamtengenezea karatasi za "political asylum" kukimbilia ughaibuni. Tafadhali bwana Lissu tunakuomba utuachie nchi yetu amani, wewe unaweza kufunga virago vyako ukafie huko ughaibuni na tuachie watoto zetu waishi kwa amani nchini Tanzania.

Anonymous said...

Wadau na mdsu mtoa mada. Seala.la Zanzibar linachangiwa saana na Serikali ya CCM bara b kwa kulenga kutaka kuendelea kutawala pale na ndicho kilichotokea. Sidhani Rais kusema hahusiki ni kweli.! Ulinzinwa jeshi kutapakaa Zanzibar na tena toka bara ni dhahiri kabisa. Mipangonya kurudia uchaguzi sio kweli walishaandaa matokeo tayari tayarikama ilivyofanyika bara. Tusitarajie kingine au miujiza kutokea. Hivyo wanasiasa wanapozungumzia jambo hili kwa vyovyote watakabiliwa iii basi wananchinwasisikie lolote. Kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM ni kielelezo tosha kutaka watakayo na kwa gharama yoyote. Lissu hana kosa kuzungumza yaliyo moyoni. Ni kwanini byama vyote visiwe na mazungumzo kuoata muafaka. Na huyu msimamizi wa tume ZEC. Jecha ni Jipu lililoiva mbona hawalitumbui. Amaninitakuwepo kwa nguvu za dola na wakiumia ninwadogo wasio na hatia. Amani napita.

Anonymous said...

tanznia kuna amani kwani? amani is ya mdomoni tu.acheni zenu

Anonymous said...

acheni kuwa na vichwa tope ambvyo hamjui hata haki zenu, akitokea mtu kuwatetea mnamuona kama katoka sayari nyengine, huyo ni mtetezi wa wanyonge. asante lissu

Anonymous said...

Lisu mtetezi wa wanyonge. Go Tundu Lisu. Pigania haki za wananchi.