ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 29, 2016

MBWANA SAMATTA APATA BAO LAKE LA KWANZA NA TIMU YAKE YA GENK CLUB VS CLUB BRUGGE


By Mwandishi Wetu, Mwananchi ___ mwananchipapers@mwananchi.co.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunga bao lake la kwanza Ulaya wakati timu yake Genk ikichapa Club Brugge kwa mabao 3-2 katika Ligi Kuu Ubelgiji.

Samatta aliyeingia akitokea benchi katika dakika 77, alitumia dakika nne tu kupachika bao lake la kwanza na kuihakikishia timu yake pointi tatu muhimu kwenye Uwanja wake wa nyumbani wa Cristal Arena. Hicho ni kipigo cha kwanza kwa vinara wa Ligi Kuu Ubelgiji, Club Brugge mwaka huu.

Club Brugge ilianza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza kupitia Thomas Meunier, lakini Genk iliamka na kupata bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika 36 mfungaji akiwa na Nikolaos Karelis, kabla ya Thomas Buffel kuongeza la pili dakika ya 50.

Samatta alipachika bao la tatu kwa wenyeji katika dakika ya 81, Club Brugge ilipata bao la pili kupitia Hans Vanaken katika dakika 83.

Hata hivyo, siku hiyo nzuri ya Samatta iliingia doa baada ya kuonyeshwa kadi njano katika dakika ya 90.

No comments: