ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 24, 2016

MSAJILI WA HAZINA AKAGUA UJENZI WA MRADI WA ECO RESIDENCE UNAOJENGWA NA NHC KINONDONI HANANASIFU

2
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akimsikiliza Violet Mafuwe Msanifu wa majengo kutoka kampuni ya CPI Iternational ambaye pia ni Meneja Mradi wa Eco Residence wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
3
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akimuuliza jambo Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu mambo mbalimbali kuhusu miradi ya shirika hilo wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
4
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
5
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo.
6
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya Msajili wa Hazina kukagua mradi huo.
8

Jengo linavyoonekana kwa nje.

Akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya ukaguzi wa jeno hilo Msajiri wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru amepongeza uongozi wa NHC kwa kazi kubwa wanayoifanya ambapo wamefanikiwa kujenga majengo yenye tahami ya shilingi Trilioni 3.5 kutoka umiliki wa mwanzo ambapo kulikuwa na majengo yenye thamani ya shilingi trilioni 1.

Mkopo uliotumika kugharamia ujenzi wa majengo hayo mapya kutoka mabenki mbalimbali ni jumla ya shilingi Bilioni 300 ambazo kiasi cha shilingi Bilioni 100 zimeshalipwa tayari katika mabenki hayo na kiasi cha shilingi bilioni 200 zinaendelea kulipwa.

Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu amesema shirika hilo linao mpango mkubwa wa ujenzi wa nyumba 500 za gharama nafuu kwa ajili ya watanzania wenye kipato cha chini ambazo zitaanza kujengwa mwaka huu huko Luguruni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)

No comments: