ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 21, 2016

MUHONGO: NCHI INAHITAJI UMEME WA UHAKIKA

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema ili Tanzania iwe nchi ya viwanda inahitaji umeme wa uhakika na nafuu.
Mara kadhaa, Rais John Magufuli amekuwa akisisitiza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ili kukuza ajira kwa vijana na kukuza uchumi.
Akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni jana, Profesa Muhongo alisema amewapa kazi Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuangalia namna ya kupunguza bei za umeme.
Alisema amewaagiza wadau hao wa nishati kumpa ripoti kamili ya namna ya kupunguza gharama za umeme na vyanzo vya kuzalisha ifikapo Machi mwaka huu.
“Lengo ni kuhakikisha tunaangalia namna ya kwenda katika uwekezaji wa viwanda huku kukiwa na umeme nafuu,” alisema.
Alisema bei ya umeme haiwezi kupungua kama vyanzo vya kuzalisha umeme havitaongezeka.
Alisema mkakati uliopo ni kuzalisha umeme wa makaa ya mawe ambao kwa sasa kuna tani zaidi ya bilioni 10 ambazo hazijaanza kuzalishwa.
Alivitaja vyanzo vingine kuwa ni nishati jadidifu ya jua, upepo, mawimbi na mabaki ya mimea.

No comments: