Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga akifungua warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA. Mwezeshaji katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka akizungumza katika warsha hiyo.
Mwezeshaji katika warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, Valeria Msoka (kulia) akizungumza katika warsha hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga (kulia) akifungua warsha ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea wanawake, vijana na watu wenyeulemavu, ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini Tanzania. Warsha hiyo iliandaliwa na TAMWA. Bi. Stella Jairos ambaye ni miongoni mwa wagombea walioshiriki Uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha hiyo. Bi. Jairos aligombea Ubunge Vitimaalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimesema wanawake waliogombea nafasi mbalimbali kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 walikosa nafasi ya kutosha kuzungumza kwenye vyombo vya habari. Alisema utafiti mdogo walioufanya katika vyombo vya habari kadhaa ulibaini kuwa ni asilimia 11 tu ya wanawake wagombea ndio walipata nafasi ya kuandikwa katika magazeti wakati wa uchaguzi huo.
Takwimu hizo zilitolewa jana katika semina ya wadau wa vyombo vya habari pamoja na baadhi ya wagombea na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Edda Sanga alipokuwa akifungua semina hiyo ambayo pia ilishirikisha wahariri kutoka vyombo anuai vya habari nchini Tanzania.
Alisema katika utafiti huo uliofanywa kwa miezi miwili yaani Septemba na Oktoba 2016 kwenye magazeti sita ulibaini kati ya vyanzo vya habari 2577 vilivyotumika kwenye habari za Uchaguzi Mkuu, wanaume waliotumika kama vyanzo walikuwa 2256 ikiwa ni sawa na asilimia 88 huku wanawake 303 kama vyanzo hii ikiwa ni asilimia 11 tu.
Mkurugenzi huyo Mtendaji wa TAMWA alisema utafiti pia uliainisha kuwa wanaume waliongoza katika makundi yote ya mada za habari hata zile ambazo hazikuwa zikihusiana na uchaguzi huo. Aliongeza kuwa katika utafiti huo ilikuwa ni nadra sana kupata habari ambazo zipo katika kurasa za mbele huku vyanzo vyake vikiwa vimetokana na wanawake. Habari za wanawake zilianza kujitokeza kuanzia kurasa za nne na kuendelea.
"...Kwa mujibu wa matokeo ya ufuatiliaji wa habari za magazeti, wanawake kwa ujumla waliogombea na wasiogombea kote nchini walikabiliwa na unyanyasaji kama vile kufanyiwa ghasia, na vitisho wakati wa kampeni na siku ya uchaguzi. Pia wanaume walificha kadi za kupigia kura za wanawake zao, wanaume waliwalazimisha wake zao kuwapigia kura wagombea ambao wanawataka hata kama mwanamke hamtaki, utumiaji wa lugha ya matusi dhidi ya wagombea wanawake na wakati wa kampeni kuna baadhi ya wagombea wanawake walikamatwa na kutishiwa kwa tuhuma za kutotii amri ya Jeshi la Polisi," alisema Sanga katika taarifa yake akifungua semina hiyo. Baadhi ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na wagombea hao.Wanahabari waliminya sauti za wanawake Uchaguzi Mkuu - Utafiti
Baadhi ya wagombea walioshiriki katika uchaguzi Mkuu 2015 wakizungumza kuelezea changamoto anuai katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na wagombea hao. Baadhi ya washiriki katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na kushirikisha wadau wa habari pamoja na baadhi ya wagombea walioshiriki katika Uchaguzi Mkuu 2015 kuzungumzia changamoto za kutopewa nafasi wagombea wanawake, vijana na walemavu kwenye vyombo vya habari.
Kwa upande wao wanawake waliogombea wakizungumza katika semina hiyo walisema vyombo vya habari kiujumla havikutoa nafasi sawa kwa wagombea hasa wanawake na vingi vilikimbilia kutoa habari za wagombea wenye majina na maarufu kwa wanajamii. Bi. Stella Jairos ambaye aligombea Ubunge Vitimaalum Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dodoma alisema wanawake walemavu mbali na kukosa fursa kwenye vyombo vya habari walikabiliwa na changamoto mbalimbali zilizofifisha mafanikio katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo.
Naye Loyce Kibona aliyegombea upande wa vyama vya upinzani katika uchaguzi huo alisema licha ya vyombo vya habari kuwa ni changamoto kwao kupata nafasi ya kusikika bado hali ya kujiamini kwa wanawake na kukatishana tamaa kunaendelewa kukwamisha mafanikio ya kundi hilo hivyo kuwataka wanawake kuungana mkono.
Imeandaliwa: www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment