Mgeni Rasmi katika ufunguzi
wa Mkutano wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF
uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu
wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu
Kijaju akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo uliowakutanisha
Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano
wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake ya Ufunguzi
huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya
katika suala zima la kuihudumia jamii, pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo
kuwakumbuka Wakulima kule vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na
kuwaingiza katika mfuko huo ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.PICHA
NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa
PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii
na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili
kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye
Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju.
Baadhi ya Wadau washiriki wa
mkutano huo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka
wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya
"Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia
mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju alipokuwa
akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa
siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Meza kuu wakati mkutano ukiendelea
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele
akijadiliana jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa Mkutano wa Mwaka
wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya
"Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia
mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12,
2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere,
Jijini Dar es salaam.
Mmoja wa wanachama wa Mfuko wa PPF mwenye ulemavu wa kusikia akiendelea kufatilia mada mbali mbali kwenye mkutano huo kupitia mkalimani wa lugha ya alama.
Wadau wakipitia kablasha la PPF.
Picha ya pamoja na washindi wa Tuzo mbali mbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akitoa hotuba fypi ya shukrani kwa niaba ya mifuko ya hifadhi za jamii nchini.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama na
wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya
hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", ulioanza leo kwenye
Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment