ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 23, 2016

PENZI LA IDRISS NA WEMA LIMEFIKA MWISHO, WEMA AMEFUTA PICHA ZOTE ZA IDRISS ALIZOWAHI KUWEKA INSTAGRAM.


Penzi donda ndugu, ndio msemo pekee unaoweza kuupachika katika kipindi kama hiki cha migogoro ya mahusiano.
Japo hatujafahamu hasa chanzo ni nini, na nini hasa kimetokea lakini dalili za awali tu zinaonesha penzi kati ya muigizaji Wema Sepetu na mshindi wa Big Brother Idriss Sultan limefika kikomo.
Vita ya maneno kati ya wawili hawa, iliibukia mitandaoni huku kila mmoja akirusha vijembe kwa mwenzake.
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mastaa hawa wamelivunja penzi lao mapema mno, huku mwanadada Wema Sepetu akionekana muhanga zaidi kwani amefuta picha zote za Idriss alizowahi kupost mtandaoni Instagram.
Matatizo kati yao yameanza kuibuka tangu siku ilipowekwa wazi kuwa, Ujauzito wa Wema umeharibika.

2 comments:

Anonymous said...

Wema unacheza na maisha wewe.tulia maisha yanaendelea hayarudi nyuma.miaka inakwenda hAirudi nyuma .tulia

Anonymous said...

Yaani huyu demu khaaa,kila kukicha ni issue tu,tulia tu na ujiheshimu,huwezi shindana na mwanaume hata siku moja,