KAMATI YA MAANDALIZU YA MAZISHI NA FAMILIA YA MAREHEMU GEORGE SEBO INAPENDA KUWASHUKURU WATANZANIA WOTE WALIOSHIRIKIANA NASI KWA HALI MALI ILI KUFANIKISHA MAZISHI YA MPENDWA WETU GEORGE SEBO ALIYEZIKWA JANUARI 30, 2016, MEDIA MBALI MBALI ZIKIWEMO VIJIMAMBO, KILIMANJARO RADIO,SUNDAY SHOMARI BLOG NA BLOG NYINGINE MBALI MBALI ZILIZOSHIRIKI KUHABARISHA JUMUIYA, SHUKRANI ZA PEKEE KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JOHN MAGUFULI KWA KUIFARIJI FAMILIA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
SHUKRANI ZA PEKEE PIA KWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA MHESHIMIWA JAKAYA KIKWETE KWA KUCHUKUWA MUDA WAKE NA KUFARIJI, SHUKRANI KWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI MHESHIMIWA WILSON MASILINGI KWA USHIRIKIANO ALIOUTOA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU KWA FAMILIA.
FAMILIA PIA INASHUKURU WACHUNGAJI VIONGOZI MBALI MBALI WA DINI VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI, WALIOITUMIA SALAAM ZA KUIFARIJI.SIO RAHISI KUMSHUKURU MMOJA MMOJA KWA JINA LAKINI KUTOKA NDANI YA MIOYO YETU TUNAOMBA MPOKEE SHUKRANI HIZI
MUNGU AWAONGEZEE, AWAZIDISHIE NA KUWAPATIA HAJA ZA MIOYO YENU.
TENA KWA NIABA YA FAMILIA TUNAWASHUKURU.
AUGUSTINO MALINDA
MWENYEKITI KAMATI YA MAANDALIZI YA MAZISH
No comments:
Post a Comment