ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 20, 2016

TASWIRA MBALI MBALI ZA MTANANGE WA YANGA NA SIMBA ULIOPIGWA JIONI YA LEO UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

Yanga imeifunga Simba kwa mabao 2-0 ikiwa ni mara ya pili katika msimu mmoja wa Ligi Kuu Bara.

Katika mzunguko wa kwanza, Yanga iliifunga Simba kwa idadi hiyo ya mabao wauaji wakiwa ni Amissi Tambwe na Malimi Busungu.

Lakini leo, Doland Ngoma na Tambwe ndiyo walioimaliza Simba na kumaliza ubishi wa mechi hiyo ya watani

GOOOOOOOOOO Dk 72 Tambwe anafunga bao kwa ulaini kabisa baada ya uzembe wa kupindukia wa safu ya ulinzi, Juuko alishindwa kumdhibiti. Tambwe aliunganisha krosi safi kabisa ya Mwashiuya

No comments: