ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 20, 2016

MWANAHABARI FRED MOSHA AFARIKI DUNIA

Habari wadau, kwa masikitiko makubwa naomba kuwajulisha kuwa mwanafamilia mwenzetu katika uandishi wa habari za michezo na burudani Fred Mosha ‘Mkuu’ amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.

Naomba tushirikiane na familia katika kipindi hiki kigumu. Marehemu alikuwa akiishi Mbagala Saku kwa Mkongo, tutajulishana kadri nitakavyopata taarifa, lakini marehemu alikuwa akifanya kazi Redio Tumaini, hivyo naamini tutapata taarifa vizuri muda si mrefu.
                                                                                                Ahsanteni,
     Katibu Mkuu TASWA
    20/02/2016

No comments: