Habari Yako Mwananchi,bila shaka ungependa kujua taarifa kuhusu klabu yako bora Tanzania!Siku ya leo nimefanikiwa kuonana na Daktari wa klabu yetu aliyedumu kwa siku 13 tu huku akishutumiwa na mwenyekiti wetu Yusuf Manji kuwa ni mwananchama wa Simba!Dr. Haroun Haroun anakusimulia mkasa mzima na mambo mengi yaliyojificha. . Indelea.
Mimi ni daktari wa michezo ambae pia nina taaluma ya Nutrution Sorts Medic (Ushauri wa matumizi ya chakula lishe kwa wanamichezo)taaluma niliyoipata nikiwa Mayotte Island nilihudumu pia timu ya wanamichezo wa Rugby kama Medical Room Manager (Daktari wa Michezo) Mayotte ni kisiwa kinapatikana Kusini mwa Tanzania chini ya mkusanyiko wa Visiwa vinne vya Comoros Island lakini Mayotte iko chini ya taifa la Wafaransa ambayo ni sehemu inayojulikana kama ni sehemu ya utawala wa Ufaransa nina kibali cha kufanya kama kazi katika Umoja wa Madaktari wa michezo Leseni grade B1 ya uhudumu wa Michezo katika nchi za ulaya .
Nimeajiajiri mwenyewe katika sekta ya usafirishaji okozi wa wagonjwa kwa njia ya anga na barabara pia kitalaamu tunaita (MEDIVAC service) Medical Evacuation, nilipata pia kuajiriwa kama Flying Doctors Meneja katika kampuni kubwa ya Bima ya afya hapa nchini.
Napenda kuchukua muda wangu kuandika hiki kitu kwa majonzi makubwa na pia huzuni nilipata kusoma taarifa ya vyombo vya habari iliyofanywa na Mwenyekiti wa timu ya Yanga Yusuf Manji katiaka maelezo yake aligusia daktari mtoa huduma wa Yanga katika mechi iliyochezwa siku ya jumamosi tarehe 12 Desemba mwaka jana Yanga ilipocheza na Mgambo Shooting katika mzunguko wa kwanza wa ligi ya VPL hapa nchini Tanzania katika kikao chake na Waandishi wa habari alisema daktari huyo ingawa jina lilihifadhiwa kwamba alikuwa ni Mwanachama wa simba na ana kadi ya uanachama.
Ningeomba kuchukua nafasi kueleza ukweli uliopo, aliyoyasema Manji hayana ukweli wowote na onaonesha mbabaishaji na wala hanijui ninemtaka kutafuta taarifa sahihi kuhusu maisha yangu na atajua kila kitu na sio kunitumia mimi kumchafua mtu ambaye kwanza alinibembeleza kwa nguvu nikubali kufanya kazi Yanga.Timu ya Yanga wakati msimu wa ligi ulipoanza mwaka jana chini ya daktari wa timu hiyo Juma Sufiani walifanya uchunguzi wa wachezaji wa yanga kabla ligi haijaanza kuna baadhi tu hawakufanya kwa kuwa walikuwa na majukumu ya kutumikia timu ya taifa lakini robo tatu ya wachezaji walifanya uchunguzi katika zoezi hilo vifaa tiba vilivyotumika vilikuwa vya kisasa na havijawahi kutumika popote Tanzania katika uchunguzi wa wachezaji na vifaa vyote vilikuwa MALI YANGU mimi na vifaa vyenye thamani zaidi ya dola za kimarekani 7500/= nilijitolea kusaidia timu ya Yanga kufanikisha zoezi bila malipo yoyote zaidi nilipewa pesa Tshs 20,000/= kama ya mafuta ya gari zoezi hilo liliendeshwa kushirikiana na TASMA (chama cha madaktari wa michezo), ambae ni katibu wa chama hicho kwangu mimi namuita ni sehemu ya upotoshaji wa taarifa ya kuwa mimi ni mwanachama wa simba na hastahili kuwa kiongozi kwa kuwa ndiye aliyekuwa akitumia nguvu nyingi kunichafua ili nafasi yangu aipate na Yanga wenyewe wanamjua juu ya tabia yake ya kuharibu mambo,anaongoza chama ambacho kinategemewa na Shirikisho la mpira wa miguu TFF, wakati hakina vifaa vyovyote tiba ambavyo vinaweza kutumika katika zoezi mbalimbali ya uchunguzi wa wanamichezo .Zoezi hilo lilikuwa la aina yake haijapata kutokea kutokana na kuwa na uhakika wa vifaa tiba vya kisasa mpaka kwenye magazeti mbalimbali ya michezo waliandika neno INTERNATIONAL wakiridhishwa na huduma hali ya juu katika zoezi la upimaji nililowafanyia Yanga, juu ya hilo gazeti kurasa ya mbele kuna picha yangu nikisimamia matumizi ya medical mashine mbalimbali ambazo mmiliki ni mimi katika zoezi hili nilishirikirikiana na madaktari mbalimbali niko na Vielelezo mbalimbali nikiwa na Mbuyu twite,Geofrey Mwashiuya, pamoja na Kpah Sherman nikiwapatia huduma mbalimbali na katika zoezi hilo nilipata majeruhi ambae alikuwa katika matibabu zaidi ya miezi miwili bila mafanikio yoyoye na mchezaji huyo ni Said Makapu kwa taaluma niliyokuwa nayo nilijipa jukumu la kumsaidia mataibabu ya kina ili aweze kufanikiwa kujiunga na wenzake nilimpa huduma maalumu ya matibabu baada ya kumfanyia uchunguzi nilikuta kuna mgando wa damu juu ya jereha alilopata kwa ndani nilimpatia tiba ya sindano aina ya Clexcan pamoja na Matibabu ya dawa pamoja na Matibabu kwa njia ya chakula alikuwa chini yangu katika session program ya matibabu kwa muda wiki tatu na kuweza kupona kabisa jereha kwa muda mchache ambao nilihaidi kama mtaalam wa tiba wa michezo kumekuwana hatari nyingi sana baadhi ya madaktari wengi wa michezo kutumia madawa makali na yasiyoruhusiwa katika guidline ya FIFA ya matibabu ya wanamichezo hapa mfano Diclofenac na baadhi za antibiotics ambazo zinaweza kumpa madhara mchezaji na kumpunguzia kabisa uwezo wake wa kucheza mpira uwanjani.Nimekuwa mchango mkubwa sana katika yanga pia chama cha madaktari wa michezo TASMA kuwatumia email mbalimbali za matumizi sahihi ya chakula Lishe pamoja na matumizi sahihi ya vifaa tiba vya michezo nimeshindwa kujiunga na chama hicho cha madaktari wa mpira kutokana na uendeshwaji wa ubabaifu na wengi kuchanganya taaluma ya daktari wa kawaida na daktari wa michezo mpaka Leo ninavyooongea katika taarifa sijaona mtu yoyote mwenye vifaa tiba sahihi vya michezo na hii ni kutokana madaktari wengi wa michezo kutoelewa Matumizi ya vifaa hivyo pamoja na elimu sahihi ya matumizi ya dawa za michezo .
Katika muda niliofanya kazi Yanga,niligundua mengi lakini naomba niweke wazi ili wanachama na wapenzi wa Yanga waelewe,Yanga inacheza mechi zake na inashinda lakini ni katika hali ya kusimamiwa na Mungu tu nasema hivi kwasababu wachezaji wengi wa Yanga inaweza kufikia hata 45% wanaichezea Yanga wakiwa majeruhi na hili linasababishwa na uongozi kutowekea maanani kuwatibu wachezaji hao ili waitumikie Yanga na wanacheza kwasababu hawataki kupoteza nafasi lakini hawako fiti kuichezea Yanga na kinachoniumiza kocha wao anajua lakini anaogopa kuwa mkali kwa uongozi akihofia ajira yake.
KASHFA YA DAKTARI KUW A MWANACHAMA WA YANGA
Wanachama wengi wa Yanga wananijua, nimekuwa mpenzi wa Yanga kabla hata sikutegemea hata siku moja naweza kuwa Daktari wa Yanga na nilikubali kusaidia yanga kuwa Daktari kama ni taaluma ninayoipenda na napenda michezo na mtu sahihi naweza kufanya kitu amabacho hakuna aliyefanya aliyepitia Yanga kama daktari watimu nilikuwa na vifaa vya kisasa vya michezo ambavyo ni mali yangu mwenyewe na nilinunua vifaa tiba hivi kutoka Mayotte ufaransa kwa gharama ya juu nikiwa na lengo kubwa la kubadili muonekano wa zamani wa madaktari wa michezo wanapokuwa wanahudumu uwanjani nategemea Yanga ni timu kubwa ya miaka nyingi yenye weledi mkubwa nisingependa hadi leo inaenda kushiriki mashindano ya kimataifa na bado daktari wa timu anakimbia uwanjani akiwa ameweka barafu katika mfuko wa Tshs 100 hii ni uchafu na kinyume na matibabu ya mpira inajulikana duniani kote kuwa matibabu ya mpira namba moja ni barafu lakini kuna vifaa maalum ya kubebea barafu na kumuhudumia mgonjwa na siyo mifuko ya Tshs 100 hii ni kutokana na madaktari hawana weledi mzuri wa kujifunza jinsi ya kuhudumu wanamichezo unaweza kuwa daktari mzuri katika matibabu mengi lakini siyo kila daktari anaweza kuhudumu michezo lahasha nilipoingia Yanga nilikuta kila kitu kinyume katika mataibabu ya michezo na wachezaji wengi walipata huduma yangu ambayo hawajaona kokote katiba tasnia hii ya michezo ya nchi yetu Tanzania kwa ushahidi huu wachezaji wengi wa yanga kila nilipowapa huduma ya matibabu walizidi kufurahia siku hadi siku na kupendekeza kuwa niwe daktari wao daima na sikuweza kuwapa matibabu kwa kuwagawa kwa kwa mafungu kila aliyestahili huduma alipata kwa wakati na kwa uhakika zaidi kilelezo cha hicho wachezaji watakuwa mashahidi.
MKASA NZIMA WA KUAJIRIWA NA TIBOROHA
Sijawahi kuomba kazi Yanga na wala kufikiria kufanya kazi katika timu ya Yanga hata upande wa mpira wa wapinzani wa simba hii ni kutokana malipo madogo ambayo nisingeweza kufurahia kazi hii ni taaluma kama kocha au mkufunzi yoyote wa michezo naweza kuwa YANGA AZAM SIMBA au timu yoyote itayoweza kumudu gharama ya malipo yangu hii taaluma yangu na unaposema mimi ni mwanachama wa simba ni kunikosea na siyo maadili mazuri katika michezo napenda kusema watu walio wengi wananifahamu nimekuwa mpenzi wa Yanga kipindi kirefu sana, niliamua kujiunga na Yanga kama sehemu yangu ya kazi na kujipa umaarufu katika kazi yangu kibiashara ingawa mshahara ulikuwa finyu sana hii ni kutokana rekodi walikuwa na madaktari wengi ambao waliona kuwa daktari Yanga siyo sehemu ya ajira na nilikubali kutokana na upenzi wa Yanga na kupenda kuonyesha uwezo wangu katika taaluma ya matibabu katika mpira na ikiwa Yanga niliajiriwa na Tiboroha kwa pendekezo lake kwa sababu kuu moja niliweza kumfanya Makapu kupona majeraha katika kipindi chenye ahadi na kutoa taarifa ya utabibu yenye kuweza kugundua ugonjwa wa mchezaji pamoja matibabu yake vielelezo vipo .Kwa mtaalamu yoyote wa michezo au kiongozi muadirifu alistahili kunipa ajira kama daktari wa timu kabla hajanipa ajira alinieleza hali halisi Yanga na Tulikubaliana nipewe chumba Maalumu cha daktari na kuweka vifaa maalumu vya matibabu ya michezo, ni aibu kubwa sana timu kama yanga haina Medical Room mpaka leo pale Jangwani na huku wakiwa na facility kubwa ya jengo lenye vyumba lukuki havina kazi,kiongozi mkubwa wa Yanga inashindwa hata kutambua umuhimu ya tiba kwa wachezaji?namshauri Manji aende hata TP Mazembe pale DR Congo akaone Mbwana Sammata alitibiwa vipi mpaka anapata mafanikio ya namna ile, nilikubali kupewa chumba cha kufanyia kazi na niliwahaidi Yanga Kutumia vifaa vyangu kwa muda wote nitakuwa kazini, hivi ni vifaa ghali ambavyo gharama yake ni zaidi ya dola ya kimarekani 16000, Idadi ya vifaa hivi hapa chini ndio nilitoa ofa ya kuvipeleka kutumika kwa pamoja kama timu ninayotumikia kama MEDICAL ROOM MANAGER , na nilifikia mbali sana kuona Yanga ingeweza kuhudumu baadhi ya wapenzi wake pale inapotokea dharula.
Hii ni orodha ya baadhi ya vifaa vya matibabu ambavyo nilikubali kuvitoa kwa ajili ya kuhudumu Yanga ambavyo kwasasa havipo na kwa viongozi wanaotambua umuhimu wa mafanikio ya klabu wangevitafuta haraka.
DIFFIBULATOR
CRYOCUFF MACHINE WITH ALL BODY PART, THIMB, HIP, ARMS, KNEE, ANKLE na sehemu zingine za viungo vya binadamu.
ICE PARK POCKET
MASSAGE BED
ECG MACHINE
COLD COMPRESSION MACHINE
GAMOW BAG
BAG FOR HYDROTHERAPY POOL hii ni kifaa maalumu cha kuweka maji ya moto au mabarafu na kuingiza mchezaji ndani ikiwa ni sehemu ya matibabu.
PATELLA HAMER
OXMETER MACHINE
Pamoja na vifaa mbalimbali vya othorpedic kwa ajili ya kuhudumia majeruhi yanapotokea
Sababu kuu mbaya ya kutuhumiwa kuwa ni mwanachama wa yanga Tiboroha alipotaka kuniajiri alijiridhisha kwa taaluma yangu ni ya ahali ya juu ni kiwango kizuri alikuwa anasababu ya kunipa ajira na sijatuma maombi ila aliniomba nimpe cv yanga ili aniajiri na nilifanya hivyo kukubali kuitumikia Yanga kama sehemu ya benchi la ufundi ila alinitaarifu kuwa kuna daktari wa chama cha mpira wa miguu ambaye ni Nassoro Mutuzya kama alimwambia kuwa mimi ni mwanachama wa simba asinipe ajira kwa angalizo pia alipiga simu kwa mwenyekiti wa mashindano Mr Isaac Chanji kusisitiza mimi ni mwanachama wa Simba hapa hali halisi ilikuwa ni ugomvi wa ajira ambayo nafasi hiyo Daktari anaejiita mwandamizi wa Yanga alikuwa mmoja anaetaka nafasi hiyo ajira napenda kukanusha kwa mwenyekiti wa Yanga ndugu YUSUF MANJI kwa habari alizotoa katika maelezo yake na waandishi wa habari za kuwa mwanachama wa simba si za kweli na amepotoshwa na Mr ISAAC CHANJI, kwa taarifa aliyopokea kutoka kwa watendaji wake namsihi Manji kabla ya kufanya ajira yoyote Yanga apende kukutana na muhusika anaetaka ajira ili kuweza kuijiridhisha mwenyewe kwa kila kitu hasa kitengo vyeti kama medical manager room nilikuwa na mengi ya kumshauri lakini hakiuwezekana , nilipokaa Yanga kwa kipindi kifupi kama MEDICAL ROOM MANAGER Yanga nilichogundua hakuna mtendaji yoyote anaependa kuwasiliana au Kuweka taarifa kwa maandishi mambo yote amabayo ni muhimu hii ndio leo tumefikia hapa, ni baadhi tu yamewekwa taarifa kwa njia ya maandishi kwa ushahidi nilipokuja Yanga nilikuta hakuna taarifa yoyote ya Mafaili ya wachezaji walivyotibiwa majeruhi kitu ambacho ni hatari kwa club kubwa kama yanga, nilienda yanga na kuomba kufungua faili ya matibabu kwa kila mchezaji ili kuweka rekodi na pamoja kufungua medical room kwa ajili ya wachezaji lakini nilionekana kituko na mtu mwenye kuchekesha mpaka baadhi ya wachezaji walisema wewe ni daktari wa aina yake tangu yanga imeanza ila huwezi kufikia malengo kutokana na viongozi wake kutokuwa na weledi wa utendaji kazi katika michezo napenda kusema kwa mara jingine kwa hili yanga walimpotosha mwenyekiti wao na inawezekana pia hata taarifa nying katika tuhuma za tiboroha zilikuwa za namna ya uongo na upotoshwaji na sitaweza sana kumlaumu Mwenyeketi wa Timu ila pia inawezekana pia Tiboroha alipenda mfumo wa kutoweka taarifa kwa maandishi na kama angeandika maandishi sababu za msingi za kunipa ajira leo lisingewepo katika kiakao cha waandishi wa habari hii ni tatizo la mfumo wa yanga mbovu sana ubadilike kuwe na taarifa ya maandishi kwa kila jambo.
ITAENDELEA . .
SEHEMU INAYOFUATA ATAZUNGUMZIA JINSI MUINGILIANO WA MAJUKUMU ULIVYO HUKU CHANJI AKITAJWA!MGOGORO WA MATIBABU YA NGOMA.
No comments:
Post a Comment