ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 15, 2016

TUMSHAURI KIJANA HUYU




Ni wiki ya tatu sasa tangu mama asafiri kwenda kwenye msiba huko nyumbani kwao, nyumbani tumebaki mimi, baba na mfanyakazi wetu wa ndani. Kwa vile mimi nimeshamaliza chuo na muda mwingi huwa nashinda nyumbani (sina kazi) nimejikuta nikiingia katika mahusiano ya mapenzi na huyu msichana wa kazi. Juzi usiku kama kawaida yangu nilienda chumbani kwake ila sikumkuta ikabidi nitege mingo ili nijue huyu msichana kaenda wapi, baada ya kama lisaa 1 nilishtuka kuona mlango wa kwa baba unafunguliwa na yule msichana wa kazi anatoka na kwenda chumbani kwake. Niliumia sana kuona kile kitendo si kwa wivu wa mapenzi bali kwa kile kitendo alichofanya baba na ukizingatia ana mke wa ndoa ambaye ni mama yangu. Wadau naombeni busara zenu kwa kuwa anachokifanya Baba sio kizuri au nimwambie mama?

7 comments:

Anonymous said...

Na hivi huyo baba kaanza,kutembea nje awezi ,kuacha umwambie usimwambie atamfukuaza msichana wa kazi .lakini ndio itakuwa tabia yake.simnajuwa nyie wanaume,mpaka liwapate ndio mtulie.

Anonymous said...

Mwambie mama yako faster but kiakili na mama yako anatakiwa atumie akili sana wakati anapomuuliza dingi yako,pole sana kaka

Anonymous said...

Kijana, sasa ni wakati wa kukomaa. Kumwambia mama nikumgonganisha tu na baba kwani mama akibanwa atasema wewe ndio ulimwambia. Ila kiukomavu. Mchukue baba yako kwa upole na kumweleza ukweli kwamba msichana amewachanganya. Alikuwa amkatalie mmoja wenu, lakini kuwakubali wote ni mchanganyiko mbaya. Kama baba ni mtu anayeelewa mtampa nafasi yakuondoka huyo binti bila fujo nyingi. Tumia usomi wako kufanya mambo yawe shwari na hapo unaweza ata ukampa mama asijejuwa kilichotokea. Maana bila shaka mama akifahamu nyote mtamumiza mama. Pia nawe ushike adabu uache kudandia magari tu bila kujuwa mwenye gari.

Anonymous said...

Wewe kijana utakuwaje uzidiwe kete na dingi? Mara nyingi wazee ni watu wenye wivu dawa ya kuisevu ndoa ya wazee wako ni wewe kutoka na huyo mdada wandani laivu dingi atakereka pengine hata kumfukuza kazi huyo mtumishi wa ndani ikifikia hapo utakuwa umefanikisha kazi moja kubwa sana ya kusevu ndoa ya wazee.

Anonymous said...

Ogea man to man na baba yako atakuelewa. katika kuongea nae tumia busara na elimu yako kuhakikisha ujumbe unafika na unaeleweka. Baba yako anaweza kuwaka lakini lazima nawe utunishe msuli kiaina ili atambue kwamba haongei na mtoto wa chekechea. Akileta ujuaji, jaribu kumgusia kidogo madhara yatakayotokea endapo mzazi mwenzake akijua. Honestly speaking, iwapo baba yako atakuelewa na kuchukua ushauri wako atakuona bonge la mtoto miongoni mwa watoto wake na atakusifu kwamba umeelimika hukumaliza tu madara ya vyuo.

Anonymous said...

Mwambie baba yako huyo msichana ni wako na achane naye kabisa. Pili mkubushe baba yako kuwa ni mume wa mama yako. Hakuna sababu ya kuwagombanisha wazazi au ku mkosesha kazi huyo msichana. Naturally, huyo msichana atakuwa anakupenda wewe lkn anatoka na baba yako kwa sababu anataka kulinda kibarua au baba yako anampa michuzi zaidi.

Anonymous said...

Mpigeni mtungo tu,lakini mwambie mama yako kimya kimya au mwambie baba yako umesikia house girl ametembea na mtu mwenye ngoma ili amuache.