Wanafunzi waliowahi kusoma miaka ya 80 katika Shule ya Sekondari ya Hegongo, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, wakicheza muziki wakati wa hafla yao ya kukumbukana iliyofanyika kwenye Mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Martine Jengo (kulia) na Mzee Hassan wakiserebuka
Mmiliki wa TSN Group, Farouq Baghoza (kulia), ambaye pia alisoma katika shule hiyo, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kumbukumbu.
Mmiliki TSN Group, Farouq Baghoza (kulia) akiwa na wanafunzi aliosoma nao katika shule ya Hegongo, Mkurugenzi wa Mgahawa wa City Sports Lounge, Benny Kisaka (kushoto) pamoja na Gerald Yambi ambaye ni mwanachama maarufu Kundi la Friends of Simba. Baghoza aliwahi pia kuwa Mwenyekiti wa Saidia Taifa Stars Ishinde.
Sasa ni wakati wa mlo
Mwanafunzi Edwin Pemba (kushoto) akiwa na Mwalimu John Sebo (katikati) aliyewahi fundisha katika Shule ye Sekondari ya Hegongo.
Aliyewahi kuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Hegongo, John Sebo akishukuru kualikwa na waliokuwa wanafunzi wake katika hafla hiyo muhimu.Kulia ni Mwanafunzi Benny Kisaka ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Mgahawa wa City Sports Lounge.
Hawa walimaliza Kidato cha Nne katika shule hiyo 1985.
Hawa walisoma katika shule hiyo na kumaliza Kidato cha Nne miaka ya tisini
2 comments:
Bongo full minyama uzembe na vitambi!dah so sad..full magonjwa..nawashauri ndugu zangu hiyo miili mliyonayo sio kabisa..acheni kula mavyakula mengi na yenye mafuta...hizo sio afya ni hatari sana kwa maisha yenu..pia mfanye mazoezi..!inasikitisha sana si wanawake si wanaume.
mdau
Brussels
Mdau umeniacha hoi,but ni kweli kabisa bongo wanakula kila kitu,nyama,bia,wali,maandazi,vitumbua chapati wanakula tu hawajali afya zao kabisa,vitambi ndio habari ya mujini,
Post a Comment