Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliokuwa umepangwa kufanyika leo katika ukumbi wa Karimjee umeingia dosari baada ya kuzuka vurugu kubwa zilizoanzishwa na madiwani wa vyama vinavyounda Ukawa, waliopinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo.
Madiwani hao wa Ukawa waliokuwa wamejiandaa kuanza kufanya uchaguzi huo, walipinga tangazo la Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuahirisha uchaguzi huo akidai kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepeleka pingamizi Mahakamani.
Ukawa walipinga kwa nguvu tangazo hilo na kubaki ukumbini wakitaka waendelee kupinga kura kwani akidi ilikuwa inatimia na kwamba hawakupata barua yoyote ya awali kuhusu pingamizi hilo.
Hata hivyo, Polisi zaidi takribani 15 waliingia ukumbini na kuwataka madiwani hao kutii tangazo la Mkurugenzi na kuondoka ukumbini. Uamuzi huo wa Polisi ulizua varangati ukumbini humo na hali ya utulivu ilivunjika kabla ya kurejea baadae.
4 comments:
Hii ni dhahiri kubwa kabisa kuwa Chama tawala kinaendeleza yale yale ya kuona kuwa wao ndio wanaweza kuongoza na kuwatumikia wananchi. Na hili lilionekana tangu mwanzo wa kuendelea kuahirisha huo uchaguzi. Uchaguzi mdogo wa namba ya watu 160 inaletewa polisi kibao na kuweka pingamizi ya lala salama. Kweli demokrasia imeuwawa na ubovu wa CCM.!! Yaleyale yanayoenda kutendeka Zanziba. Hata Ugandaa tumeyaona kweli Africans politics ni mbovu.
Ondoka.
The video is clear hata hawa Ukawa ovyo kabisa. Iwapo kuna zuio la Mahakama na ccm imechekewa kumleta taarifa fujo zinamsaidia nani? Demokrasia bado hatuiwezi. The opposition are no angels either. Wanataka tu wao kufanya nchi haitawaliki ili kuonyesha Magufuli kashindwa. Childishness and stupidity.
Hmmmm! Kazi kweli kweli...pole pole ndio mwendo
Post a Comment