Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kizungumza na Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa (hawapo pichani) juu ya kuwawezesha viongozi katika ngazi ya Mitaa kusimamia na kulinda maeneo ya wazi ,miundombinu na maeneo mengine ya umma.( Katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi na kulia ni Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Profesa.John Lupala
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwaonesha Ramani Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa
Sehem ya Madiwani na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa wakiwa katika mkutanohu uklio fanyika jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi amesema serikali inaanza zoezi la kutambua na kubomoa nyumba zote zilizojengwa kinyume na utaratibu hasa zile zilizoziba barabara na mitaro na itaanza na miji minne ikiwemo jiji la Dar es Salaam.
Lukuvi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhi ramani za maeneo ya mitaa yote ya jiji kwa watendaji na wenyeviti wa mitaa ili kila mwananchi ajitambue eneo alilojenga kama hakustahili kuwepo aanze kujipanga.
Baadhi ya mameya waliohudhuria makabidhiano hayo mbali na kuelezea mipango ya manispaa zao juu ya suala la mipango miji wamesema baada ya wizara kutoa ramani hizo tatizo sugu la migogoro ya ardhi litapungua kwani kila mmoja atafuata taratibu na sheria zilizopo.
Wilaya ya Kinondoni ni miongoni mwa wilaya zinazodaiwa kuongoza kwa kuwa na migogoro mingi ya ardhi ambapo afisa mipango miji Bi Juliana Letara amesema asilimia 70 ya maeneo bado hayajapimwa wala kurasimishwa hali inayochangia manispaa hiyo kukosa mapato.
No comments:
Post a Comment